WEKEZA KATIKA MICHEZO KWA USTAWI WA ELIMU NA VIWANDA TANZANIA ni kauli mbiu ya michezo ya UMISETA NA UMITASHUMTA mwaka 2017, mashindano haya yanafanyika katika ngazi za wilaya, mkoa na kitaifa na kwa wilaya ya Tunduru mashindano haya yalianza katika ngazi ya Kata, Tarafa ili kupata wawilikilshi watakaoiwakilisha wilaya katika mkoa na baadaye taifa.
Akizungumza na washiriki katika ngazi ya wilaya mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji ndg George Mbisigwe Afisa Elimu Msingi Takwimu na Vifaa alisema kuwa maandalizi yamefanyika ya kutosha na wanafunzi wako tayari kwenda kushindana ngazi ya mkoa.
Aliendelea kusema kuwa wanafunzi watashiriki katika michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na mpira wa pete, mpira wa miguu,mpira wa wavu, na riadha.
Aidha ununuzi wa vifaa vya michezo vyote vimenunuliwa na maandalizi yote yamekailika hivyo anawataka washiriki kwenda kushindana na kuhakikisha wanarudi na ushindi katika michezo yote.
washiriki wamejiandaa vizuri kwani walianza kambi kuanzia tarehe 03 hadi terehe 06 june 2017 katika shule ya sekondari tunduru, ambapo waliitimsha jana na kupatikana washiriki wa ngazi ya mkoa.
Hata hivyo Halmashauri ya wilaya ya Tunduru inatarajia kuwapeleka washiriki katika ngazi ya mkoa watao 56, wakiongozwa na walimu 5, daktari na viongozi wa timu 3 ndio wataanza safari tarehe 07/06/2017 kuelekea Songea ambako yatafanyika mashindano kimkoa.
"tunatarajia kkwenda kuungana na timu nyingine za mkoa wa Ruvuma ambapo kila halmashauri ya wilaya itakuwa na wawakilishi hivyo lengo letu ni ushindi na tunaenda kushindana" alisema afisa elimu takwimu na vifaa wilaya.
Ndg Mbesigwe alisema kuwa mashindano katika ngazi ya mkoa yatafanyika kuanzia 07 june na kumalika 10 june 2017 na mchujo utafanyika ili kupata wachezaji watakaoshiriki mashindano katika ngazi ya kitaifa yakayofanyika Mkoani Mwanza kuuwakilisha mkoa wa Ruvuma.
timu ya wanafunzi na walimu wao wakiwa katika picha ya pamoja mapema wiki hii wakati wa maandalizi ya kujiandaa kwenda kushiriki michezo ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa, ambapo jumla ya washiriki 56 wataiwaikilisha Halmashauri ya wilaya ya Tunduru katika mashindano yatakayodumu kuanzia tarehe 07 june hadi 10 june 2016 ngazi ya mkoa mkoa kupata mchujo wa wachezaji wataowakilisha mkoa wa Ruvuma kitaifa mkoani mwanza.
timu ya wanafunzi wa shule za msingi wilayani tunduru watakaoshiriki katika michezo mbali mbali ya mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa, timu ina jumla ya wachezaji 56 watakaocheza michezo ya Mpira wa Miguu, Mpira wa pete, mruko ambapo kuna mruko wa juu na wa chini, pia riadha ambapo kutakua na mbio fupi na ndefu, mbio zitakua kuanzia mita 100 hadi mita 1500, mitupo ya mkuki,tufe na visahani. wanatarajia kushindana na wachezaji kutoka halmashauri zote nane za mkoa wa Ruvuma kuanzia terehe 07 hadi 10 june 2017.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.