Katika mwendelezo wa kusherekea maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibari kupitia Idara ya Afya kitengo cha Ustawi wa Jamii leo Ijumaa tarehe 28/05/2023 imeweka Kambi Shule ya Sekondari Frank westone imendelea kutoa Elimu kwa jamii kuusu aina mbalimbali za Ukatili unaoendelea kwenye Jamii yetu ikiwemo kukemea tendo la Ushoga na Usagaji.
Akiongea Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Tunduru Bi. Blandina Sekela alisema”Ukatili ni tendo lolote lile ambalo anafanyiwa mtu ambalo litamuhathili Kisakolojia ,Kimwili,Kijamii na Kiuchumi ili uitwe Ukatili ni lazima Mtu amfanyie Mtu mwenzake”.
“Kuna aina Mbalimbali za Ukatili ikiwemo Kupigwa,Kuchomwa Moto,Kukatwa mwili,Kusukumana,Maneno ya kejeli kama Shoga,Demu,Buzi N.k yote ni hayo ni Ukatili,Pia ninawaeleza Ukweli Watoto wangu wa Frank Westone la Ushoga na Usagaji havikubaliki kabisa katika Jamii kwani kwa Watoto wa Kiume vitawasababishia Madhara makubwa sana mbele ya Safari kwahiyo kwa mwanafunzi yeyote ambae ataona kuna dalili ya rafiki yake zinaonyesha anashiriki Vitendo hivyo basi atoe taarifa katika kitengo cha Ustawi wa Jamii au kwa Mwalimu yeyote wa Jirani kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi huyo” alisema Blandina.
Mwl Donald Kjasembe Katibu wa Smaujata alisema”Wanaume na Wavulana tujitaidi kutunza malinda yetu maana kwa Mwanaume akiruhusu kutolewa malinda ni hari ya hatari kwani mwanaume ni kichwa cha familia kwa kamwe tusikubali kuleft group na kuruhusu Wajanja wachache kutufanyia Ukatili huo pia mtu yeyote akifanyiwa ukatili hatakiwi kukaa kimya bali anaweza kwenda kutoa taarifa kwenye kituo cha Afay,Polisi au Kwenye Ofisi za Ustawi wa Jamii”.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.