Katika hatua kubwa ya kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Wilaya ya Tunduru, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Andrea Mathew, ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji Msechela-Liwanga. Mradi huu utakaogusa maisha ya maelfu ya watu, unatarajiwa kukamilika kwa Zaidi ya Shilingi bilioni 3.02.
Akizungumza na Wananchi katika hafla hiyo, Mhandisi Kundo alisema kuwa mradi huu ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania wanapata huduma bora ya maji safi na salama. Aliongeza kuwa mradi huu utanufaisha zaidi ya watu elfu tisa ambayo ni idadi kubwa ya wananchi wa maeneo hayo.
"Mradi huu ni ushahidi wa dhamira ya Serikali ya kuwekeza katika sekta ya maji. Tunatarajia kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huu, wananchi wa eneo hili watakuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa matumizi ya kila siku," alisema Mhe.Mhandisi Kundo.
Kwa upande wao, wananchi wa Msechela-Liwanga wameipongeza Serikali kwa kuwajengea mradi huo ambao unatarajiwa kutatua changamoto ya uhaba wa maji ambayo wamekuwa nayo kwa muda mrefu. Wamesema kuwa mradi huu utawawezesha kupata muda mwingi wa kufanya shughuli nyingine za maendeleo badala ya kupoteza muda mwingi kutafuta maji.
Mradi huu unaotekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Ruvuma, unatarajiwa kumalizika mnamo tarehe 28.02.2025, na pia, unatarajiwa kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo haya, ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakikabiliwa na uhaba wa maji.
Pichani ni Meneja wa RUWASA Tunduru, Mhandisi, Maua Mgala akitoa ufafanuzi wa Mradi wa Maji wa Misechela-Liwanga
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.