• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

MHE. Hairu Mussa apongeza hati safi Tunduru

Imewekwa : May 24th, 2024

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Mhe. Hairu Mussa, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Pongezi hizi zilitolewa katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya tatu, kikao kilichofanyika mei 24, 2024.

Aidha, Mwenyekiti ametaja Mafanikio ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ikiwemo  kufikia lengo la ukusanyaji mapato hadi kufikia Asilimia 108, robo ya tatu, pia Kujenga soko la madini ya vito ambapo wanunuzi wote watakuwa wanafanya biashara katika eneo moja.

“Mafanikio haya katika Halmasahuri ya Wilaya ya Tunduru, yanatokana na juhudi zetu madiwani , tukishirikiana na Wataalamu wetu, kwahiyo tunatakiwa kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuwa na Maendeleo endelevu”.Alisema Mhe. Hauru.

Katika kikao hicho, wajumbe wa baraza walipokea taarifa mbalimbali kutoka kwa kamati za kudumu za halmashauri kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2024. Taarifa zilizowasilishwa ni pamoja na zile za Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Ukimwi, na Kamati ya Maadili.

Afisa Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma, Ndg. Amandus Chilumba, pia aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa usimamizi bora wa ukusanyaji wa mapato. Aliwasisitiza wataalamu wa halmashauri kushirikiana vyema na madiwani ili kuhakikisha halmashauri inakuwa na maendeleo endelevu, hasa katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Simon K. Chacha, aliwasilisha salamu za Serikali, ambapo Alisisitiza jukumu la madiwani kuwa mstari wa mbele katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao ya utawala.pia aliwataka madiwani kubuni vyanzo vingine vya mapato vitavyowezesha Halmashauri kuinuka Zaidi katika Maendeleo.

Aidha, aliwataka pia kusimamia na kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shule wanapata chakula wanapokuwa shuleni, kwani hii itaboresha uwezo wao wa kujifunza.

Akifunga Kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mhe. Hairu Mussa amewapongeza Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya  Halmashauri kufikia Zaidi ya asilimia 100, amewataka wataalamu  kuendelea kutekeleza majukumu yao ili  Wilaya ya Tunduru iweze kusonga mbele kwa maendeleo.

Mafanikio haya ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru yanaonyesha dhamira ya uongozi na wafanyakazi wake katika kuhakikisha matumizi bora ya fedha za serikali na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.