Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassimu Majaliwa Majaliwa amefanya ziara ya kikazi katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru na kutembelea mradi wa ukarabati wa madarasa na mabweni ya shule ya wavulana Tunduru Secondsry iliyopo katika kata ya majengo,kijij i cha muungano ambapo mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 90 .
Aidha kutokana na lisala ambayo ilisomwa na mkuu wa shule hiyo ya Tunduru secondary ambapo katika lisala hiyo liliombwa gari la shule ambapo litakuwa likisadia wanafunzi wa shuleni hapo katika shughuli mbalimbali ikiwemo kuwasaidia wanafunzi ambao ni wagonjwa na kuwakimbiza hospitali ya wilaya kwa upande wa Mh. Waziri mkuu alimwagiza DED Tunduru kuhakikisha anapeleka gari haraka iwezekanavyo katika shule hiyo kongwe ya secondary.
Pia Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Kassimu Majaliwa Majaliwa alikagua majengo ambayo yalikarabatiwa yakiwemo madarasa na mabweni na kutoa pongezi kwa uongozi wa shule na kamati yote ya ujenzi ya shule na kuwahaidi kuwa amelizishwa na kasi ya ujenzi wa ukarabati wa madarasa na mabweni unaoendelea na kuwahakikishia kuwa ataongeza bajeti ya kukarabati nyumba za walimu baada ya ukarabati huo wa sasa wa mabweni na madarasa kukamilika ambao umeghalimu milioni mia saba tisini na mbili.
Aidha Mh. Kassimu Majaliwa Majaliwa Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania amewataka Wanafunzi,Walimu na jamii yote inayo ishi kuzunguka maeneo hayo ya shule kutunza majengo hayo ambayo serikali ya awamu ya tano ya Dkt John Pombe Magufuli imetumia fedha nyingi sana ili kugharamia miundombinu hiyo ya Elimu
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.