Mwenge wa uhuru Umepokelewa leo septemba 2 ,2021 ,katika mkoa wa Ruvuma katika wilaya ya tunduru katika kijiji cha nakapanya , sauti moja ukitokea katika mkoa wa Mtwara , mwenge wa uhuru umekabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jeneral Elisha Gaguti na umepokelewa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia jeneral barozi Willbert Ibuge pamoja na mkimbiza mwenge mkuu luteni Josephina mwambashi. Mwenge wa uhuru utapitia na kukagua miradi mbalimbali katika mkoa wa Ruvuma ,ukianzia katika wilaya ya Tunduru.
Katika wilaya ya Tunduru ,mwenge wa uhuru unakagua mradi wa maji ya RUWASA ,na kufungua zahanati katika kijiji cha Muhuwesi , na kufungua majengo ya shule ya wavulani Tunduru(TUNDURU SECONDARY), pia na kufungua mahabara ya kompyuta katika chuo cha Natembo.
Mwenge wa uhuru utashinda katika wilaya ya Tunduru hadi septremba 3 ,2021 katika kijiji cha namwinyu na kukabidhiwa tarehe hiyo hiyo wilaya ya Namtumbo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.