TUNDURU KUANZISHA DARASA LA KISOMO
Mkuu wa wilaya ya Tunduru mh.Juma Zuberi Homera afanya ufunguzi darasa la kisomo katika za msingi Mbesa na Airport zilizopo kata ya Mbesa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Akitoa hotuba kwa wanakisomo hao mh Homera alisema kuwa elimu ya watu wazima itasaidia wanakisomo kupata haki zao za msingi ikiwa watakujua kusoma,kuandika na kuhesabu hivyo kuondokana na adui ujinga katika taifa la Tanzania.
Pia kwa wananchi kupata elimu hii amabyo waliikosa kwa muda mrefu itasaidia hata katika uchaguzi wa mwaka 2020 kushiriki na kumpigia kura kiongozi unayemtaka bila ya kushawishiwa na mtu yeyote kutokana na kujua kusoma na kuandika ili kuongeza tija na kuendana na kauli mbiu ya serikali ya uchumi wa kati ifikapo 2025 haina budi kuwaelimisha wananchi wetu.
"niwasihi wananchi wote na niwaambie kuwa elimu haina mwisho na niwaambie na wale ambao bado hawajiandikisha wajitokeze ili kufuta adui Ujinga katika jamii ya wananchi wote, Elimu ni haki ya kila mtanznia" alisema mkuu wa wilaya ya Tunduru.
Afisa Elimu watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi Ndg Mussa Nkolabigawa akitoa taarifa ya mpango wa elimu wa watu wazima siku ya ufunguzi wa darasa la kisomo lilifunguliwa katika kata ya mbesa katika shule za msingi Mbesa na Airport zilizopo wilaya ya tunduru mkoani Ruvuma kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Mh.Juma Zuberi Homera.
HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU YAPATA MAKAMU MWENYEKITI
Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya tunduru mh mfaume wadali ameendelea kukitetea kiti chake baada ya kumuangusha katika uchaguzi mpinzani wake mh alhasa diwani wa kata ya tinginya kwa kujinyakulia kura 37 dhidi ya 16, uchuguzi huo ulifanyika tarehe 27/07/2017 katika mkutano mkuu wa mwaka.
makamu mwenyekiti wa halmashauri Mh. Mfaume Wadali diwani wa kata ya Namakambale akiwashukuru waheshimiwa madiwani kwa kumuani na kumpa tena nafasi ya kuwa mwenyekiti kwa mwaka mwingine baada ya mkurugenzi mtendaji (W) kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
wadali alisema " nawashukuru sana waheshimiwa madiwani kwa kuniamini na kunichagua kwa nafasi hii nyeti na muhimu ya makamu mwenyekiti naahidi kushikiriana nanyi nyote bila ya kujali itikadi za vyama vyetu na nitatumia utashi wangu kumshauri mwenyekiti katika masuala hasa ya kuindeleza halmashauri yetu na kufikia malengo kusudiwa tulijiwekea kwa mwaka wa fedha 2017/2018"
CHUO KIKUU HURIA KUFUNGUA TAWI -TUNDURU
Hayo yamesemwa na makamu mkuu wa chuo kikuu huria nchini dk Elifasi Bisanda wakati akitoa hotuba kwa wananfunzi tarajili na wale wanaoendelea na masomo katika ngazi mbali mbali katika chuo kikuu huria waliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru.
kutokana na umbali mrefu kutoka tunduru hadi kufika katika kituo cha kufanyia mtihani Songea na kuona mahitaji ya wakazi wa tunduru ni makubwa aliamua rasmi kuanzia tarehe 29/07/2017 tunduru kuwa kuwa na tawi shirikishi la chuo kikuu huria Tanzania ( The Open University of Tanzania)
aidha mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh. Juma Homera aliushukuru uongozi wa chuo kikuu huria kuanzisha tawi katika wilaya ya Tunduru kutokana na uhitaji mkubwa wa watumishi kutaka kujiendeleza lakini walishindwa kutoka na kutokuwepo kwa taasisi za elimu ya juu, vilevile umbali kutoka tunduru hadi kufika songea lilipo kilipo kituoi cha mitihani ni takribani km 265 na jeografia yake kutoka sehemu moja hadi nyingine ni ngumu hivyo kuleta usumbufu kwa wanafunzi.
Makamu mkuu wa chuo kikuu huria nchini prof:Elifasi Bisanda akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh. Juma Homera wakati alipohudhuria katika zoezi la kuanzishwa kwa kituo kishiriki cha chuo hicho wilayani Tunduru.
BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA MUSWADA WA MFUKO WA ELIMU.
Muswada wa kuanzishwa kwa mfuko wa elimu wilaya uliwasilishwa na Afisa Kilimo Ndg Chiza Marando wilaya kwa niaba ya Mkurugenzi mtandaji katika mkutano wa mwaka wa baraza la madiwani ulifanyika tarehe 27/07/2017 katika ukumbi wa klasta ya mlingoti wilaya ya tunduru mkoani ruvuma.
akiwasilishwa muswada huo ndg chiza marando alisema halmashauri ina changamoto kubwa sana ya miundombinu ya elimu kutokana na madarasa mengi kuwa mabovu, na yamejengwa kwa muda mrefu sana hivyo kusababisha wanafunzi kusoma chini ya miti, na kuwa mlindikano katika vyumba vya madarasa na katika kukabiliana na changamoto hiyo halmshauri imeamua kukata shilingi hamsini 50 katika kila kilo moja ya korosho katika msimu wa mwaka huu ili kupunguza tatizo la miundombinu katika shule.
waheshimiwa madiwani, wakuu wa idara na wananchi wakisikiliza hoja ya kuazishwa kwa mfuko wa elimu wilaya wenye lengo la kuboresha miundombinu ya shule, ikiwa ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo na ujenzi wa hosteli.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.