MEI MOSI YALETA FARAJA KWA WAFANYAKAZI
Wafanyakazi wilayani Tunduru wameungana na wafanyakazi Tanzania na duniani kote katika kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi ambayo hufanyika kila mwaka mei mosi,siku ya wafanyakazi wilaya ya Tunduru ilianza kwa maandamano kutoka idara ya ujenzi hadi uwanja wa mpira wa miguu Wilaya, na kufuatiwa na ushereheshaji ulioambatana na vikundi vya Sanaa za maonesho na michezo mbalimbali.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi Mh Juma Zuberi Homera wakati wa maadhimisho ya kiwilaya mratibu wa sherehe za Mei Mosi ambaye pia ni katibu wa chama cha wafanyakazi Wilaya Ndg Kassimu Dean alisema wafanyakazi wanakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwa ni pamoja na makato makubwa ya kodi, mishahara midogo isiyokidhi hali halisi ya maisha kwa sasa, malimbikizo ya mshahara na kutotambulika kwa waendesha pikipiki kama kazi rasmi.
Akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi Wilaya iliyanyika katika viwanja vya mpira mgeni rasmi ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh Juma Zuberi Homera aliwapongeza wafanyakazi wote kwa utumishi uliotukuka na uwajibikaji hasa katika kutekeleza maagizo mbali mbali ya serikali kwa wakati katika kuwahudumia wananchi na hasa katika kutatua kero za wananchi kutekeleza dhana ya utawala bora.
Mh. Homera aliendelea kusema kuwa Madai,Haki na Stahiki mbali mbali za watumishi amezichukua na anauagiza uongozi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini kuwasilisha malalamiko hayo kwa Raisi wa Jamuhuru ya muungano wa Tanzania Mh.Jonh Joseph Pombe Magufuli kwa majadiliano ili kutafutiwa ufumbuzi.
Serikali itaendelea kulipa madeni mbali mbali ya watumishi kadiri ya makusanyo yake kutokana na zoezi la uhakiki na kuwaondoa wafanyakazi hewa serikalini limekamilika.
“baada ya zoezi la uhakiki kuisha kinachofuata ni raisi kuongeza viwango vya mshahara kwa watumishi, haki na stahiki zote zitalipwa kulingano na mapato ya nchi”alisema mh Homera.
Aidha alisema kuwa usafiri wa pikipiki unatambuliwa kisheria lakini anasikitishwa sana na baadhi yao kutimiwa na majangili katika kusafisha meno na pembe za ndovu, wengine wananshikiana na majambazi katika kutekeleza uhalifu.
Mh Homera aliendelea kusema kuwa serikali haitawafumbia macho wananchi wanaotumia usafiri huo kuvunja sharia za nchi na sharia za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na maderava pikipiki wanaobeba mishikaki ambayo kisheria ni marufuku.
“kwa muendesha pikipiki (bodaboda) wanaotumia usafiri huu vibaya waache mara moja kwani sharia itachukua nafasi yake endapo utakamatwa, baadhi yenu mnashirikiana na majambazi kwa kutumia pikipiki zenu pia” alisema mkuu wa wilaya ya Tunduru.
Hata hivyo alimalizia kwa kutoa zawadi za vyeti na Hundi kwa wafanyakazi hodari kwa mwaka 2017 waliofanya vizuri katika katika utendaji wa kazi katika kada mbalimbali kutoka katika idara na sekita mbali mbali za umma na binafsi Wilayani Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.