“Michezo, sanaa na Taaluma ni msingi wa maendeleo ya mwanafunzi katika taifa letu”ni kauli mbiu ya mashindano ya UMISSETA (Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania) kwa mwaka 2018 ambayo kitaifa yatafanyika jijini Mwanza.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mchangani Fatuma Chalamanda alisema kuwa mashindano ya UMISSETA ngazi ya wilaya yanashirikisha wanafunzi kutoka tarafa saba za halmashauri ya wilaya ya Tunduru, ambazo ni tarafa ya Mlingoti, Nalasi, Lukumbule,Namasakata, nampungu, Matemanga na Nakapanya.
UUMISSETA kwa mwaka 2018 una jumla ya washezaji 219 kati yao, wavulana 130 na wasichana 89, wachezaji hawa wanatarajiwa kupiga kambi kwa muda wa siku tatu katika shule ya sekondari Tunduru wakishiriki mashindano mbalimbali ili kupata timu ya Wilaya.
Mwalimu Chalamanda alitaja michezo wanafunzi watakayoshindanishwa kuwa mbio ndefu mita 1500 na fupi mita 100 na 400 kwa wavulana na wasichana, mpira wa miguu, mpira wa pete,mpira wa wavu,mpira wa kikapu na mpira wa mikono kwa upande wasichana pekee, miruko na mitupo pamoja na fani za ndani kama ngoma, kwaya na ngonjera.
Mwalimu Makina akifanya utambulisho wa viongozi na walimu wakuu, walimu wa michezo waliambatana na wanafunzi kushiriki katika mashindano ya UMISSETA ngazi ya wilaya yanayofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Tunduru kuanzia tarehe 19 hadi 21 mei 2019
Akitoa hotuba ya ufunguzi wa michezo ya UMISSETA ngazi ya wilaya mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Zuberi Homera alianza kwa kutoa pongezi kwa wanafunzi na viongozi walioshiriki katika kufanya maandalizi kuanzia ngazi ya kata hata hadi kufika wilaya.
“nawapongezeni mlichaguliwa kushiriki mashindano ya UMISSETA ngazi ya Wilaya kwani mlikuwa wengi sana ambao mlioshirikikkatika ngazi ya shule na Kata” alisema Juma Homera.
Pia Juma Homera alitoa wosia kwa wanamichezo kuwa waende kufanya kazi wanayotumwa na wilaya ya kwenda kushindana na sio ushiriki, na muda wa kuonesha vipaji vyenu ni katika mashindano kama haya.
Aidha Juma Homera aliwaambia washiriki wa UMISSETA ngazi ya wilaya kuwa katika michezo kuna mambo matatu ya msingi ya kuzingatia kwa kila mchezaji anayetaka mafanikio, ambayo ni Nidhamu, Tabia Njema,kujituma na kuhudhuria mazoezi kila siku.
Hata hivyo alisema michezo haitaishia katika mashindano ya UMISSETA tuu, lahasha wilaya imeandaa utaratibu wa kuanzisha Timu ya MPira wa Miguu ya Wilaya Itakajulikana kama Tunduru Korosho United itakayokuwa na wachezaji kutoka katika kila Tarafa, hivyo wanafunzi watakaokuwa wamemaliza kidato cha nne ndio watakuwa wadau wa timu hiyo.
mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera akitoa Hotuba ya Ufunguzi wa mashindano ya UMISSETA ngazi ya wilaya mapema leo.
“Tuko kwenye mchakato wa kuanzisha timu ya Tunduru Korosho football Club, na watakaokuwa wanacheza vizuri baada ya kumaliza kidato cha nne ndio watakuwa wachezaji, na tutafanya mchakato wa kupata wachezaji kutoka kila Tarafa”
Aidha Juma Homera alifanya harambee ya kupata fedha za kuwezesha ya kuwaunga mkono wachezaji watakaosafiri kwenda kushiriki michezo ngazi ya mkoa na taifa na jumla ya shilingi milioni 1,560 000 zilichangiwa,fedha taslimu zilikua 260,000 na ahadi 1,260,000.
Aliendelea kutanabaisha wanafunzi wasifikirie michezo tuu, wazingatie masomo ili hali ya ufaulu wilayani Tunduru kiweze kupanda na kuondoa kabisa daraja sifuri kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018.
Naye mwakilishi wa kaimu mkurugenzi halmashauri ya Tunduru Ndg Juma Ally alimshukuru mgeni rasmi na kuwakumbusha wanafunzi wafanye kilichowaleta kambini ni michezo na sio mambo mengine, aliwaasa kufanya michezo kwa nidhamu ya hali ya juu ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza.
wanafunzi washiriki wa UMISSETA ngazi ya wilaya wakipita kwa maandamano mbele ya Mgeni rasmi kabla ya kuanza kwa halfa ya ufunguzi wa Mashindano hayo ngazi ya wilaya
“niwaase wanafunzi mmekuja kufanya michezo angalieni msije mkaondoka na mimba kambini au mkapatwa magonjwa kama ukimwi kwani maambiki sio lazima kutoka kwa watu wazima bali hata vijana na watoto wengine wana matatizo hayo” alisema Juma Ally mwakilishi wa Mkurugenzi.
Hata hivyo mgeni rasmi alifungua mashindano hayo kwa namna ya pekee ya upigaji wa penati kuashirika kwamba michezo ya UMISSETA imefunguliwa rasmi wilayani Tunduru kuanzia tarehe 19/05/2018.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.