Makamu mwenyekiti wa Tunduru dc Ndg Said Ally Bwanali akiongea na wanafunzi wa shule mpya ya Mindu Sekondari ambayo imepata usajili mwezi wa Tatu 2021 ambapo Makamu mwenyekiti wa Tunduru dc amewataka Wanafunzi hao wasome kwa bidii maana dunia ya sasa Elimu ndie mkombozi katika Maisha yao.
Aidha Makamu mwenyekiti amewapongeza Viongozi na Wananchi wote wa kata ya Mindu kwa kuamua kujenga shule yao ya kata ambayo kwa sasa imesha sajiliwa na wanafunzi wameanza kusoma makamu mwenyekiti amewapongeza kwa Majengo mazuri waliyo ya jenga katika shule hiyo ya sekondari uku Halmashauri ikiwasaidia kwa 70% na uku 30% ikiwa ni nguvu ya Wananchi wa Mindu.
Pia Makamu Mwenyekiti amewataka Wananchi na Wanafunzi kwa ujumla wajitaidi kutunza miundombinu ya shule hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu zaidi maana gharama iliyo tumika ni kubwa katika kujenga miundombinu hiyo hivyo kila mwananchi anawajibika kulinda mali za shule hiyo.
Aidha Makamu Mwenyekiti amezitaka kata ambazo hazina Sekondari zijitaidi zijenge shule za kata pia amesema uongozi wa kata hizo ambazo hazina sekondari zianzishe mradi wa ujenzi wa sekondari za kata kama watashindwa waende wakajifunze kwenye kata ambazo zimefanikiwa lengo ni kuwa Kata zote 39 za Halmasha ya wilaya ya Tunduru ziwe na Sekondari za kata.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.