Mafunzo ya mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania yanayofadhiliwa na SIDA (Shirika la maendeleo la Sweden) kupitia Shirika la hifadhi ya Mazingira Duniani (WWF) yanafanyika katika kijiji cha Mkowela Wilayani Tunduru kwa mfululizo wa siku tatu 02-04 mwezi Januari.
Pichani Mbele, Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira, Bwn. Dunia Almas akiwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yanalenga kuboresha ufuatiliaji wa uwajibikaji katika jamii, vile vile, kuimarisha ushirikiano wa vikundi vya mtandao huo kwa manufaa ya usimamizi endelevu wa misitu nchini Tanzania. Mafunzo hayo yamekutanisha makundi manne, ambayo ni;Halmashauri ya Kijiji, kamati ya maliasili,Jamii wenye ushawishi na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Aidha, Baada ya mafunzo kumalizika, makundi haya manne yanatarajiwa kuwa na uwezo wa kutoa elimu kwa wana jamii wote juu ya usimamizi wa matumizi ya Rasilimali za umma.
Mradi huo utatekelezwa kwa miaka mitano, kuanzia 2023-2028.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.