Hayo yameshwa na meneja wa benki ya NMB tawi la Tunduru Ndg Goodluck Shirima alipokuwa akizungumza na wakuu wa Idara na Vitengo alipotembelea ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kwa ajili ya kutoa taarifa ya marekebisho ya mikopo kwa watumishi wa umma.
Ndg shirima alisema hapo awali kabla ya maboresho mkopo kwa watumishi wa Umma ulikua na Riba ya asilimia 19 ya mkopo lakini baada ya maboresho yaliyofanyika riba sasa itakuwa ni asilimia 17 ya mkopo kwa watumishi waliopo katika mamlaka za serikali za mitaa (LGAs).
Meneja wa NMB tawi Tunduru Ndg Goodluck Shirima (wa kwanaza kushoto)akiwa katika kikao na wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru mapema wiki cha kutoa taarifa ya maboresho ya mikopo kwa watumishi wa umma.
Aliendelea kusema maboresho mengine yaliyofanyika ni pamoja na kuanzishwa kwa bima kwa mkopaji ambayo itakuwa ni asilimia 0.75 ya mkopo, hii itasaidia benki kuweza kurejesha deni endapo mkopaji atapata ulemavu wa kudumu utakaosababisha ashindwe kuendelea na majukumu yake au kifo.
Ndg Goodluck Shirima alisema kuwa kiwango kabisa cha mtumishi wa umma kukopa ni shilingi laki na kiwango cha juu kabisa kwa mtumishi ni shilingi milioni 50 kulingana na kiwango chake mshahara na umri alionao kazini.
Ndg Shirima alisema sifa za mtumishi kupata mkopo kutoka benki ya NMB ni pamoja na viambatanisho vifuatavyo barua ya ajira, hati ya malipo ya mshahara (current salary slip), kopi ya kitambulisho cha kazi, barua ya uthibitisho kazini, barua ya utambulisho na picha za pasipoti za kivuli cha rangi ya bluu.
Aidha alisema benki ya NMB huduma ya mikopo ya nyumba kwa watumishi ambapo mtumishi anaweza kukopa hadi milioni 700 kulingana na kipato chake na kujenga nyumba ya ndoto yake kwa kipindi cha muda mfupi.
Akizungumza kuhusu marejesho ya mkopo wa NMB ndg Shirima alisema kuwa mkopo wa nyumba wa NMB unaweza kurejesha kwa kipindi cha hadi miezi 71 ukilinganisha na ilivyokuwa awali kabla ya maboresho, pia mtumishi unaweza kuchukua mkopo na kufanya ujenzi sehemu yeyote ndani ya ardhi ya Tanzania.
wakuu wa idara na vitengo wakiwa katika kikao na uongozi wa NMB tawi la Tunduru
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Tunduru Ndg Jonathani Albano Haule aliwashukuru Benki ya NMB tawi la Tunduru kufika kutoa taarifa za maboresho lakini watumishi watatumia fursa iliyotolewa na benki katika kufikia malengo yao.
Kaimu Mkurugenzi alimalizia kwa kusema kuwa wana uhakika elimu iliyotolewa kwa wakuu wa idara na vitengo itawafikia watumishi walio wengi wenye sifa za kukopa, kupitia wakuu wao taarifa zitakuwa zimewafikia watumishi wote.
Theresia Mallya.
Afisa Habari Tunduru DC.
0764287387
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.