Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Tunduru Bw.Augustino Maneno akiwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Masonya kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru amezindua Mradi wa Madarasa 10 ambao wenye Thamani ya Tzs 200,000,000/= ni fedha ambazo zimetolewa na Mh.Dkt Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bw.Augustino Maneno Kaimu Katibu Tawala Wilaya akiongea na Wadau Mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi huo wa Madarasa alisema”Kwanza napenda kutoa Shukurani zangu za dhati kwa Mh.Dkt Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia Wilaya ya Tunduru Milioni 200 kwajili ya mradi wa Madarasa 10 ya Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ambapo hadi sasa madarasa yote yamekamilika 100% na yapo tayari kwa matumizi yaliyokusudiwa”.
”Uku fedha tolewa Milioni 200 zilipelekwa katika Shule za Sekondari Masonya mradi wa Darasa 1,Matemanga Sekondari mradi wa madarasa 3,Semeni sekondari mradi wa Madarasa 2,Nakapanya Sekondari mradi wa Darasa 1,Kidodoma Sekondari mradi wa Darasa 1,Misechela Sekondari mradi wa darasa 1 na Ligoma Sekondari mradi wa Darasa 1, jumla tunapata madarasa 10 yenye thamani ya milioni 200 pongezi pekee kwa Mama Samia yeye ni mlezi bora ndio maana alitupatia hizo fedha kwajili ya kujenga madarasa ya kukalia kidato cha kwanza” Alisema Das Maneno.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.