Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imesherekea sikukuu ya Muungano wa Tangayika na Zanzibari kwa Kufanya Usafi wa Mazingira katika Kituo cha Afya Masonya ambapo kituo hicho ni moja kati ya Vituo Vipya vilivyo Jengwa na Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha gharama za mradi huo wa kituo cha Afya Masonya ni Milioni 500 mradi umefikia 95% ambapo kwa sasa vinasubiliwa vifaa tiba tu kwajili ya kuanza kutoa huduma kwa Wananchi, uku Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Tunduru Bw.Augustino Maneno akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tunduru amewataka Wananchi wa Kata ya Masonya wajitaidi kutunza mazingaira ikiwemo kufanya usafi mara kwa mara na Kupanda miti kwajili ya Kivuli kwa Wagonjwa pale wanapofika kituoni hapo kwajili ya kupata matibabu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.