Kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima yamefanyika kitaifa katika mkoa wa Ruvuma wilayani tunduru tarehe 21/09/2019 ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala mkoa wa Ruvuma Ndg Hassan M Bendeyeko aliyemuwakilisha Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknilojia Mh.Eng Stella Manyanya.yenye kauli mbiu ya kisomo katika Ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia kwa maendeleo ya nchi.
Alisema katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 mkoa wa ruvuma ulikuwa na jumla ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika wapatao milioni 72,713 na kwa tunduru peke yake ni 32,330 ndio sababu kubwa ya serikali kufanya maamuzi ya kuleta maadhimisho haya katika wilaya ya tunduru ili kuleta msukumo kwa wananchi kujuiunga na elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi kwa waliokosa.
Mgeni rasmi aliendelea kusema nchi inapoelekea kwenye uchumi wa kati na viwanda yapo madhara mengi yatakayolikumba taifa kama wananchi hawatakuwa wanajua kusoma, kuhesabu na kuandika kwani kuna mabadiliko makubwa sana ya sayansi na teknolojia yanayaojitokeza kwa kasi na ili kuendana nayo wananchi wanatakiwa kuwekeza katika elimu na kupata wataalam waliobobea katika fani tofauti tofauti.
Alisisitiza jamii ya watanzania wasiojua kusoma, kuhesabu na kuandika kujitokeza kwa wingi na wasione haya kwani wanakosa fursa nyingi na haki zao kutokana na kukosa stadi hizo, kwani serikali ya mkoa wa ruvuma ilijiwekea malengo hadi kufika 2020 kupunguza au kufuta kabisa tatizo la ujinga kwa wananchi wake.
Mgeni rasmi aliziagiza maafisa elimu wa mikoa yote nchini wa tanzania bara na hata visiwani kuhakikisha kuwa wanaanzisha madarasa ya elimu ya watu wazima kote nchini tunapoelekea katika uchaguzi mkuu 2020 tuhakikishe kuwa wananchi wetu wananjua kusoma na kuandika ili kuondoa udanganyifu unaweza kutumika kutokana na dhana ya usiri kupotea kwa sababu kutokujua kusoma na kuandika.
Alimalizia kwa kupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya tunduru kwa usimamizi mzuri katika sekta ya elimu kwani wamekuwa na muamko mkubwa sana katika elimu alisema "mwaka 2012 wilaya ya tunduru ilikuwa inashika nafasi ya mwiisho kimkoa na ufaulu wake ulikuwa asilimia 91.9 lakini wamefanya jitihada na sasa ufaulu umepanda hadi kufikia asilimia 67.7 kwa mwaka 2015 katika matokeo ya mtihani ya darasa la saba na kidato cha nne pia.
pia mgengi rasmi alikabidhi zawadi za ngao na vyeti kwa shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne kwa Halmashauri zote nane za mkoa wa Ruvuma, za Nyasa, Mbinga tc, Mbinga dc, Madaba, Songea manispaa, Songea vijiji, Namtumbo na Tunduru
Aidha aliwataka wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote bara na visiwani kusimamia utekelezaji wa elimu ya watu wazima katika maeneo yao ya utendaji kwani wananchi wanapokuwa na uelewa inakuwa njia rahisi sana kwao kuweza kupata haki zao, kufanya usimamizi wa maendeleo ya watoto wao mashuleni, kuwa na uwezo wa kuhoji na kudai haki zao za msingi na hata kushiriki katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kujiletea maendeleo kwa mtu mmoja mmoja.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.