Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ilishiriki Bonanza la michezo na Taasisi ya Mbesa Mission, ikiwa ni Maadhimisho ya kumbukumbu kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, katika viwanja vya Mbesa Mission.
Halmashauri ya wilaya ya Tunduru iliwakilishwa na timu ya Kurugenzi SC na taasisi ya Mbesa iliwakilishwa na CMML SC ,michezo mbalimbali ilichezwa ikiwemo Mpira wa Miguu, Mpira wa Wavu ,Mpira wa Pete , Mchezo wa bao na mchezo wa draft.
Pichani ni wachezaji wa Kurugenzi SC (wenye jezi nyeupe) wakishiriki Mpira wa Wavu.
Katika michezo yote hakupatikana mshindi wa Jumla kwani timu zote mbili zilifanikiwa kushinda michezo mitatu kati ya sita iliyochezwa, aidha katika mchezo wa Mpira wa Miguu Kurugenzi SC ilikubali kipigo cha Goli 1 dhidi ya CMML SC goli pekee lililofungwa na mshambuliaji wa CMML SC Nathanael Chilijila katika kipindi cha kwanza.
Aidha, katika michezo mingine ikiwemo Mpira wa pete Kurugenzi SC iliifunga CMML SC Goli 11 – 1, na mpira wa wavu Kurugenzi Fc kushinda kwa seti 2 kati ya seti 3 zilizopangwa kuchezwa, katika mchezo wa Bao Kurugenzi SC ilishinda michezo miwili kati ya mitatu iliyochezwa kwa upande wa draft kushindwa kwa michezo miwili dhidi ya CMML SC.
Akishukuru kwa niaba ya timu, Afisa Maendeleo ya Michezo Ndg, Abdilahi Namkopo amesema michezo ni sehemu ya kutengeneza mahusiano yenye tija miongoni mwa jamii, na kuhimiza kuwa uhusiano huu uliowekwa kuwa endelevu.
“Michezo ujenga umoja,ushirikiano na upendo baina yetu, kwahiyo kwa upande wetu tunashukuru kwa ukarimu mkubwa mliotuonyesha na kuhaidi kudumisha ushirikiano huu “. Alisema.
Kurugenzi SC inatarajia kuwaalika pia CMML SC katika mchezo wa marudiano utakaochezwa viwanja vya nyumbani, ambapo tarehe ya Mchezo huo bado haijapangwa.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.