Katika mnada wa tatu wa korosho kidodoma afisa ubora wilaya ya Tunduru ndg Mustapha Mohamed makumbuli alieleza ubora wa korosho zinazolimwa katika wilaya ya tunduru kuwa ni korosho bora na kuthibitisha kuwa mwaka uliopita korosho zilizozalishwa wilaya ya tunduru zilishika nafaasi ya kwanza kwa ubora kulinganisha na wilaya nyingine zinazozalisha zao hilo.
Aidha afisa ubora aliwapa elimu wakulima wa kidodoma juu ya kuweza kuthibiti tatizo la korosho kutokuwa na kitu ndani kwa jina maarufu alitaamka “MBWAWA”
Afisa ubora wilaya aliwasihi wakulima kuwahi kuokota korosho pindi tu zinapodondoka na kila baada ya siku tatu kuhakikisha wanaenda kuokota korosho hizo, pia kuanika korosho zao kabla hawajazipeleka sokoni
Pia aliwasihi wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu katika uchangaji wa madawa au viuatilifu vya kuboresha zao hilo la korosho.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.