Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro, akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru Mh. Sanga Milongo,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Tunduru ndg. Masanja Kengese, wakuu wa Taasisi mbali mbali, wakuu wa Idara pamoja na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru wameazimisha Kilele cha Zoezi la Usafishaji wa mazingira Duniani.
Katika zoezi hilo, Viongozi walishirikiana na wananchi katika kufanya usafi wa mazingira wakianzia Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru na maeneo mbali mbali ya Wilaya, ikiwa ni pamoja na barabara, mitaro, sokoni na maeneo ya biashara.
Akizungumza na wananchi waliotikia zoezi la usafishaji wa mazingira Mh. Mtatiro ameagiza idara ya mazingira kuhakikisha penye makutano ya mitaro kukaguliwa, kufanya kikao na wafanyabiashara wote ili kubaini changamoto zilizopo ndani ya siku 14.
“Usafi sio kazi ya Serikali na uchafu hauna kisingizio, mitaro ilindwe na ifanyiwe usafi, wekeni utaratibu wa kusimamiana ili yeyote anaemwaga uchafu ovyo kwenye mitaro ashughulikiwe, uchafu unadhibitika, niwaombe tusaidiane kuiweka Tunduru yetu katika hali ya usafi”. Alisema.
Akifafanua hilo Mh. DC Mtatiro alisema, Serikali imetimiza wajibu wake kujenga miundombinu ya Barabara na mifereji, hivyo amewaasa wananchi wawajibike kutunza mazingira yao.
Aidha ametoa agizo zoezi la usafi liwe endelevu, wafanyabiashara wote wawe na vifaa vya kuweka taka,vile vile, kila jumamosi ya mwisho wa mwezi iwe siku ya usafi, viongozi wa halmashauri watakuwa wakipita maeneo yote kwa ajili ya kuhimiza wananchi kufanya usafi.
Zoezi la usafishaji wa mazingira duniani kote lilianza mnamo Septemba 11, 2023, na kuhitimishwa mnamo Septemba 16, 2023, kauli mbiu ikiwa “Tuungane pamoja ,kujifunza,kupanga na kuhimiza uimalishaji huduma za udhibiti wa Taka"
Imeandaliwa na Orpa Kijanda,Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.