Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kupitia wajumbe wa kamati ya lishe wamekutana kujadili na kupanga bajeti ya lishe 2023- 2024 ambapo katika kikao hicho cha bajeti kiliudhuriwa na Afisa lishe mkoa Bi.Anna Nombo.
Bi.Anna Nombo alisema”katika swala la lishe katika Halmasharui ya Tunduru ilifanya vizuri kulingana na ukubwa wa eneo la kiutawala uku akitoa wito kwa wadau wa kilimo kuhamasisha jamii walime vyakula vyenye virutubisho kama vile mahindi ya njano, Maharage , matumizi ya maziwa freshi na watoto wanyonye maziwa ya mama adi miezi sita baada ya kuzaili bila kumlisha chochote”.
Pia amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma zitenge bajeti ya kutosha kwajili ya maswala ya lishe ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kutengea bajeti kubwa ya Milioni mia moja thelathini ambayo ni zaidi ya bajeti ya mwaka unaoishia ambayo ilitengwa milioni sabini tu.
Kwa upande wa Halmashauri akiongea Afisa Mipango “nawataka Wakuu wa iadara na Vitengo ukifika wakati wa kutekeleza bajeti ya lishe kila mkuu wa idara na kitengo hakikishe anatenga bajeti ya kutosha kwenye swala la lishe pia aliwaomba watumishi wa idara ya kilimo watoe elimu ya kutosha kwa wakulima wa Tunduru walime mazao ambayo yatasaidia upatikanaji wa lishe Tunduru utakuwa rahisi na kwa bei zuri tofauti na sasa bei ya vyakula lishe ipo juu kutokana uletwa kutoka nje ya Tunduru”.
Mwisho. Afisa Mipango aliwataka Wakuu wa idara na vitengo utekelezaji ukafanyike kwa Vitendo lengo katika bajeti 2023-2024 Tunduru tumejipanga kuitekeleza kwa 100% bila kikwazo chochote kile.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.