Akiwa katika ziara ya siku mbili wilayani Tunduru mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme ametembelea mradi wa uzalishaji wa umeme jua unaotekelezwa na kampuni ya power corner katika kijiji cha Lukumbule kwa shilingi milioni 849,455,600.00 unaotaraji kutoa huduma kwa wananchi wapatao 600 utakapokamilika.
Akiwa katika kituo cha uzalishaji wa umeme jua cha kampuni ya power corner Bi. Mndeme alitoa pongezi kwa kampuni hiyo kuunga mkono juhudi za serikali za kuwaletea maendeleo wananchi na kusogeza huduma karibu na wananchi.
Aidha aliwataka wananchi wa kijiji cha Lukumbule kuchangamkia fursa hiyo ya Umeme Jua katika kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kuongeza kipato “ni fursa sasa ya kufungua viwanda vidogo kama vya kutengeneza juice, seremala, saloon”
Mitambo ya Uzalishaji Umeme jua iliyosimikwa katika kijiji cha Lukumbule, yenye uwezo wa kuzalisha Umeme jua wa Msongo wa kilowatts 40.2
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo meneja mradi wa power corner kanda ya kusini alisema kituo cha uzalishaji Umeme Jua kina uwezo wa kuzalisha Umeme wenye Msongo wa Kilowatts 40.2 wenye uwezo wa kusambazwa kwa wananchi au wakazi zaidi ya 500 katika kijiji cha Lukumbule, hadi octoba 2018 kampuni imeunganisha umeme kwa wananchi wapatao 141 kati ya 400 ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za kijamii mojawapo ikiwa Umeme.
Aliendelea kusema kuwa kampuni ya power corner ina miradi ipatayo 14 kwa nchi nzima lakini kwa mkoa wa Ruvuma wapo katika halmashauri ya Tunduru kutoa huduma katika kijiji cha Lukumbule, Misyaje na Marumba ili kuendana na sera ya uchumi wa kati ifikapo 2025 na serikali ya viwanda wananchi hawana budi kupelekewa nishati ya umeme karibu.
Meneja mradi wa Power Corner kanda ya Kusini akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Ruuvuma Bi. Chritina Mndeme baada ya kusoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Umeme Jua.
Alisema miongoni mwa faida ambazo mwananchi /mteja atapata ni pamoja huduma ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao, wananchi kuanzisha viwanda vidogo,mafundi seremala kutumia nishati ya umeme katika kazi zao na kutoa elimu kwa watoto wadogo katika kituo cha power corner kwa njia ya runinga kwa kutumia CD za ubongo kids.
Hata hivyo power corner imeahidi kufunga umeme katika pampu ya kusukuma maji Lukumbule ili kurahisha gharama za uendeshaji za mradi huo ambao kwa sasa umesimama kutokana na wananchi kushindwa kuchangia gharama uendeshaji wa jenereta la Diseli.
Imeandaliwa
Theresia Mallya
Afisa Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.