Katibu Tawala Wilaya ya Tunduru Ndg. Milongo Sanga ametoa cheti cha pongezi kwa kata ya Kidodoma, ambayo imefanya vizuri katika usimamizi wa afya na lishe katika robo ya kwanza (Julai Septemba 2023) , Novemba 06, 2023 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imefanya kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa afya za Lishe ngazi ya wilaya na jamii , Lengo ikiwa ni kuona mwenendo wa Lishe katika maeneo ya wilaya ya Tunduru, ili kujua hatua zipi ziendelee kuchuliwa kudhibiti viashiria vya Lishe kwa kipindi cha Robo ya kwanza (Julai Septemba 2023) kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Ndg. Milongo Sanga ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho cha Tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa afya za lishe ngazi ya wilaya, kilichohudhuliwa na watendaji kata wa wilaya ya Tunduru, Ndg Milongo Sanga aliwasisitiza Watendaji kuendelea kusimamia masuala ya lishe kwani ni agenda ya kitaifa, kwa maeneo ambayo hayajafanyi vizuri zaidi kuendelea kusimamia viashiria hivyo nakuona vinafanya vizuri katika maeneo yao ya usimamizi.
Pichani ,Katibu Tawala Wilaya ya Tunduru Ndg. Milongo Sanga akizungumza katika kikao cha Tathmini ya Lishe robo ya kwanza, ambapo alikua Mwenyekiti wa kikao hicho.
“Lishe ni muhimu sana katika maeneo yetu kwani linachukuliwa kwa ngazi ya Taifa, kwahiyo watendaji twende tukasimamie viashiria vyote ili afya za wananchi wetu zizidi kuimarika Alisema.
Aidha kwa upande wake katibu wa kikao hicho cha Tathmini ya Lishe Ndg. Chiza Marando ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, amewataka watendaji kuzidi kuonesha ushirikiano kwa idara ya afya hasa katika sekta ya Lishe ili kuinua asilimia za usimamizi wa afya na Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Pichani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndg. Chiza Marando (Aliesimama) akizungumza wakati wa kikao cha Tathmini ya lishe, Ambapo alikua katibu wa kikao hicho.
Kitengo cha Lishe katika kuhakikisha inatatua changamoto nyingi za Lishe inaendelea kuhamasisha viwanda vidogo vya kuchakata chakula kuingia mikataba na SANKU kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa virutubishi katika vyakula hivyo, pia kuhamasisha upatikanaji wa mbegu ziliongezwa virutubishi. SANKU ni wadau wa lishe ambao wanafanya Mradi wa uongezaji virutubishi katika vyakula hasa wakati wa uchakataji wa vyakula hivyo.
Pichani , baaadhi ya Watendaji wa kata zilizopo Wilaya ya Tunduru Katika Kikao cha Tathmini ya Lishe Robo ya kwanza.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.