Na Theresia Mallya-Tunduru
23/05/2019
Mnada wa kwanza wa zao la ufuta umeendeshwa leo wilayani Tunduru katika Tarafa ya Lukumbule ambapo jumla ya makampuni sita yalijitokeza kununua zao hilo na jumla ya Tani 239 sawa na kilogramu 239,000 zilinunuliwa na kampuni ya Sunshine limited ya dar es salaam kwa bei ya shilingi 3080 kwa kilogramu moja.
Akifungua mnada wa ufuta Halmashauri ya Tunduru kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Tunduru Ndg.Gasper Zahoro Balyomi aliwapongeza wananchi wa wilaya ya Tunduru kukubali kuuza mazao katika vituo maalum kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ili kumkomboa mwananchi kiuchumi.
Ndg.Gasper Balyomi aliwaambia wananchi wa wilaya ya Tunduru kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine waziri mkuu na makamu wa rais wanawapongeza sana kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kulima mazao ya kimkakati kama Ufuta na Korosho.
Aidha alisema serikali imeanzisha mfumo huu stakabadhi ghalani wa kuuza mazao katika vituo maalum kwa lengo la kila mwananchi kupata bei nzuri na kupambana na biashara za magendo zenye lengo la kumkandamiza mkulima.
Mkurugenzi huyo alifungua mnada wa kwanza Halmashauri ya Tunduru tarehe 23 mei 2019 uliofanyika katika kijiji cha lukumbule wilayani tunduru, huku akiwapondegza wananchi wa lukumbule kwa ushirikiano walioonesha kujitokeza kwa wingi katika mnada ambazo jumla ya Tani 239 sawa na kilogram 239,000 zitauzwa katika mnada wa hadhara.
Na kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Tunduru ndg.Mussa Manjauli aliipongeza serikali kuitia bodi ya mazao mchanganyiko kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kwa zao la ufuta kwani utaongeza tija kwa wakulima.
Pia wakulima wa wilaya ya Tunduru watapata fursa ya kujiendeleza kiuchumi kwani kilimo kinachofanywa na wananchi wa tunduru kinategemeana wanapovuna ufuta na kuuza vizuri wanapata fedha kwa ajili ya kununua pembejeo za zao la Korosho.
“naipongeza serikali kwa kuweka usimamizi wa zao la Ufuta na kuingizwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani kwani msimu wa kilimo uliopita wakulima waliuza holela na kupata kiasi cha shilingi 2300 kwa kilo lakini katika msimu tunaona matunda makubwa kwani mnada wa kwanza tuu umeanza kwa shilingi 3080 na kujitokeza kwa wanunuzi wenye uhakika ukilinganisha na huko nyuma” alisema Ndg Mussa Manjauli Makamu Mwenyekiti wa TAMCU.
Wananchi wa Lukumbule waliishukuru serikali kusimamia vizuri zao hilo na kuhakikisha kuwa mkulima anapata tija kwa kazi anazofanya, huku wakioomba serikali kusimamia katika malipo ili yafanyike kwa wakati kwani wengi wanategemea fedha za ufuta kwa ajili ya kununua viatilifu vya Korosho.
Bw.Mussa Amuri Chama “alisema mwaka jana ufuta uliuzwa kwa bei ya shilingi 2300 lakini sasa hivi tumeuza kwenye mnada shilingi ufuta ni shilingi 3080 tunaipongeza serikali kwa kweli lakini tuaomba maboresho yafanyike katika upatakanaji wa mbegu za kisasa na pembejeo kwa wakati”
Wananchi wengi wanafanya kilimo cha mazao kama sehemu ya chakula lakini ili kuendana na sera ya serikali ya kuinua uchumi wqa wananchi hadi kufikia kipato cha kati ifikapo 2025 imeamua kuweka nguvu katika usimamizi wa kilimo ili kiwe na tija kwa wakulima.
Mwisho
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.