Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imefanya uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Nchini kuanzia Tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba 2023.
Katibu tawala Wilaya ya Tunduru Ndg.Milongo Sanga alikuwa Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tunduru. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, ambapo aliwasihi wadau kuendelea kuwa Mabarozi wazuri katika kupinga ukatili katika jamii, pia kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria vitendo vyote vya ukatili kwa mamlaka zinahusika na kudhibiti ukatili wa kijinsia.
Aidha, Katibu Tawala amesema katika kutimiza lengo la kampeni hiyo, juu ya kupinga vitendo vya ukatili katika jamii, yapaswa kuzingatia na kuungana na asasi za kijamii katika kuelimisha, kuhamasisha,kukemea na kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa jinsia katika jamii.
"Tukiyazingatia haya,ni hakika kabisa ukatili katika jamii zetu, wilaya na Taifa kwa ujumla utapungua kwa kiasi kikubwa"
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Tunduru Bi.Brandina Sekela alizungumza kuhusu muongozo wa kampeni hiyo ya siku 16 katika kupinga ukatili,ambapo amesema lengo kuu la kampeni hii ni kuungana na wadau, kupata nguvu ya pamoja katika kuhimiza na kushawishi jamii kutokomeza vitendo vya ukatili wa jinsia ili kufikia usawa wa kijinsia.
Sambamba nae Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Letesia Mwageni,amezungumza juu ya shughuli zilizofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru katika kuendelea kupinga ukatili wa kijinsia katika Jamii, hasa kwa kundi la wanawake ambalo lipo katika hatari kubwa ya kunyanyasika.
Kampeni hiyo imezinduliwa Novemba 25 katika Mkoa wa Dar es salaam, na kilele chake kitakua Disemba 10, 2023, aidha kampeni hiyo inatakiwa kufanyika katika ngazi zote kuanzia ngazi ya Vijiji/Mtaa, Kata na Halmashauri , ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu inasema "WEKEZA: Kuzuia Ukatili wa kijinsia".
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.