Kamati ya ulinzi wa wanawake na Watoto wilayani Tunduru wachagizwa kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili kuleteleza uelewa wa pamoja katika jamii ya usawa wa jinsia na vita ya ukatili dhidi ya wanawake na Watoto.
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto halmashauri ya wilaya ya Tunduru wakati wa kufunga mafunzo yaliyodumu kwa muda wa siku tatu Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya tunduru ndg Chiza Cyprian Marando amesema Mafunzo haya yamekuja wakati sahihi kwani vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinaendelea kila siku katika jamii na hakuna mtu wa kuwasemesea.
Ndg marando aliendlea kusema kuwa kumekuwa na kamati nyingi sana zinaanzishwa kwa ajili ya kulinda haki za watoto na wanawake lakini zinakuwa sio endelevu lakini atahakikisha kuwa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji na ukatili inafanya kazi yake ili kwenda kubadilisha jamii ya Tunduru. "Imekuwa ni kawaida kuanzishwa kwa madawati mengi ya masuala ya jinsia ambayo yanakuwa hayafanyi kazi yake, lakini kwa kamati hii ya ulinzi wa wanawake na watoto dhidi ya unyanyasaji na ukatili inatekeleza majukumu yake, na kila mjumbe kufanya katika sehemu yake kutoa elimu kwa jamii"
vile vile Ndg Chiza Marando aliendelea kusema kuwa Tunduru inakumbana na changamoto ya mila na desturi potofu ambazo zinasababisha ukosefu wa usawa wa kijinsia na zaidi hata katika malezi kwa watoto kuwa ni magumu sana hivyo kwa kuanzishwa kwa kamati hii kutasaidia kupunguza kabisa matatizo ya malezi na makuzi ya watoto.
Pia kamati hii itapata fursa ya kwenda kutoa elimu kwa jamii, ambayo inabadilisha kabisa mtazamo wa jamii kupunguza janga la ndoa za utotoni na mimba mashuleni
Kaimu Mkurugenzi halamashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg Chiza Cyprian Marando akiongeza na washiriki wa mafunzo ya kamati ya ulinzi wa wananwake na watoto halmashauri ya Tunduru wakati wa kufunga mafunzo yaliyodumu kwa muda wa siku, katika ukumbi wa hospitali ya wilaya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.