Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Tunduru ikiongozwa na Cde. Abdallah Mtila imetembelea majimbo ya Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini kukagua miradi ya maji mwezi Novemba, 27.
Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Ndaje - Mbesa (Vijiji vya Mbesa, Lijombo na Airport), tarafa ya Nalasi, Mradi wa Misechela (Misechela na Liwanga), tarafa ya Namasakata, Mradi wa Maji kata ya Majimaji tarafa ya Nakapanya, Mradi wa Maji kata ya Masonya, tarafa ya Mlingoti, miradi hiyo ni miongoni mwa miradi mingi ya maji inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Kamati hiyo iliyoambatana na wajumbe wake ilitumia zaidi ya kilomita 389 kukagua na kujionea ufanisi wa miradi minne ya maji yenye thamani zaidi ya Shilingi Bilioni 4.8. Ukaguzi wa miradi hiyo ni katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo ni serikali ya awamu ya sita.
Aidha, Kamati imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Daktari, Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Maji, RUWASA, viongozi wote na watendaji kwa juhudi kubwa za kuibadilisha wilaya ya Tunduru.
Miradi hiyo inatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Tunduru ndani ya miaka 5 ijayo,ambapo, kutokana na ukubwa wa miradi hii na mawanda yake, matatizo ya maji yatakuwa yamemalizwa kwa asilimia 90 kwenye wilaya kubwa.
Ukaguzi huu wa miradi unasaidia kutambua mapungufu yoyote katika utekelezaji wa miradi, na hatua za kurekebisha mapungufu hayo huchukuliwa mara moja. Ukaguzi huangalia utekelezaji wa miradi ya maendeleo hiyo kwa kuzingatia mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uwiano wa gharama na kazi iliyofanyika, ubora wa vifaa na kazi zilizofanywa, muda wa utekelezaji wa mradi na matumizi sahihi ya fedha za mradi.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.