Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Tunduru, Miradi hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) lililopo katika Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa Shule mpya, maabara, majengo ya Tehama, mabweni,na vyoo. Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa, Mhe. Komred Oddo Mwisho, na iliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali, Labani Thomas.
Pichani (aliyeshika koleo): Mwenyekiti wa kamati ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa, Mhe. Komred Oddo Mwisho.
Baada ya kukagua miradi hiyo, Kamati iliridhika na utekelezaji wake. Komred Mwisho aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo, na pia aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kusimamia vyema utekelezaji wa miradi hiyo. Alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo umekuwa wa kuridhisha na unakwenda sambamba na maelekezo ya Serikali.
"Tumefurahishwa sana na utekelezaji wa miradi hii. Tunaipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo. Tunaamini kuwa miradi hii itasaidia kuboresha hali ya maisha ya wananchi wa Tunduru, Kwa kipindi kirefu watoto wetu wamekua wakipata shida kwasababu Shule zilikua mbali sana, lakini mpaka sasa karibia kila kata inapata shule” alisema Mhe. Mwisho. “Tunawapongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kusimamia vyema utekelezaji wa miradi hii. Tunaamini kuwa ushirikiano huu utaendelea kuwepo ili kufanikisha miradi mingine ya maendeleo,"
Aidha, kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali, Labani Thomas, aliipongeza Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa kwa kufanya ukaguzi wa miradi hiyo. Na kuwa ukaguzi huo ni muhimu ili kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango, aliahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Ruvuma. Alisema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii.
Pichani: Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Labani Thomas
"Ninaipongeza Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa kwa kufanya ukaguzi wa miradi hii. Ukaguzi huu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango “. Alisema “Tutaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Ruvuma, ni wazi kwamba Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Daktari. Samia Suluhu Hassan, ina dhamira ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii,"
Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma katika wilaya ya Tunduru ni sehemu ya ziara inayoendelea katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.