na Theresia Mallya-Tunduru
20/05/2019
Viongozi naombeni msimamie ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri zenu ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea katika bajeti na kutekeleza mipango iliyop kwenye mpango wa bajeti wa mwaka 2018/2019 alisema Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Tunduru Ndg.Augustine Maneno wakati akifungua mkutano wa Jumuiya Tawala za Mitaa ALAT Mkoa wa Ruvuma uliofanyika wilayani Tunduru.
Ni wakati wa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuacha kutegemea katika mazao tuu kwani katika msimu mwaka 2018/2019 tumekutana na changamoto ya ukosefu wa masoko hivyo mkoa wetu kushindwa kufikia malengo.
Akitoa mfano wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ambayo kwa kiasi kikubwa mapato ya ndani inategemea katika mazao ya Korosho, Mbaazi na Mpunga Ndg Augustine Maneno alisema “korosho imenunuliwa na serikali hivyo Halmashauri za Tunduru na Namtumbo wamekosa mapato eneo hilo, ni wakati sasa kila Halmashauri kubuni vyanzo mbadala vya mapato badala ya kutegemea mazao ya kilimo pekee”
Mdau wa uzalishaji wa mbegu bora za Muhogo kutoka Shirika la MEDA akitoa maelekezo ya namna ya uandaaji wa shamba kwa wajumbe wa ALAT mkoa wa Ruvuma walipotembelea shamba la Mkulima mzalishaji wa mbegu Ndg Athmani Nkinde.
Kaimu Katibu Tawala huyo aliendelea kwa kuwataka wajumbe wa ALAT wa Ruvuma kusimamia na kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ya utawala ili iwe na ubora na kuzingatia thamani ya fedha iliyotolewa, kwani serikali imetoa fedha nyingi sana zinazohitaji kutoa matokea chanya.
Aidha aliwataka wajumbe hao wanaporudi katika Halmashauri zao kuanzisha mpango mkakati wa benki tofali kwa kila kijiji ili kukabiliana na kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa na kuboresha mazingira ya kujifunzia wanafunzi.
Alisema “tukiboresha miundombinu ya kujifunzia hata wanafunzi watapenda shule na kusoma kwa furaha, kama wakipenda shule basi hata kiwango cha ufaulu kitaongezeka katika shule za mkoa wa Ruvuma”
Kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Tunduru Bi Celestina Kahangwa ambaye pia ni Afisa Elimu Sekondari akitoa taarifa fupu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa maktaba katika shule ya sekondari Masonya wakati wa ukaguzi wa miradi uliofanywa na wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa mkoa wa Ruvuma siku moja kabla ya kufanya Mkutano wa kujadili maendeleo ya mkoa wao.
Aliwakumbusha wajumbe kuwa sera ya serikali ya awamu ya Tano katika sekta ya Afya ni kila kijiji kuwa na zahanati ili kurahisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi, nendeni mkawahamasishe wananchi kufyatua tofali na kuanza ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji.
Kaimu Katibu Tawala alimalizia kwa kuwataka wajumbe wa ALAT mkoa wa Ruvuma kuwaalika wadua mbalimbali wanaotoa huduma katika mkoa wa Ruvuma katika vikao na mikutano ili kutoa elimu ya namna wanavyotoa huduma kwa wananchi kwa ajili ya maendeleo mapana ya mkoa wa Ruvuma.
Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa walifanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika shule za sekondari Masonya ,ujenzi wa maktaba, Frankweston ukamilishaji wa maboma 2 na shamba la uzalishaji wa mbegu bora za mhogo aina ya Kiroba lilipo kata ya sisi kwa sisi wilayani Tunduru.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.