Maandalizi ya maadhimisho ya juma la Elimu Watu Wazima wilayani Tunduru yaendelea kwa Afisa Elimu Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo rasmi kutembelea vituo vya elimu ya watu wazima kuzungumza na wanakisomo juu ya maandalizi na umuhimu wa maadhimisho hayo katika wilaya ya Tunduru
Afisa Elimu watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi Mwalimu Musa Nkolabigawa alisema maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima huadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 01 septemba hadi 08 kila mwaka kidunia lakini kitaifa maadhimisho haya yatafanyika tarehe 21 ikiwa ndio kilele na itafanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Tunduru.
alisema maadhimisho haya yana kauli mbiu ya "KISOMO KATIKA ULIMWENGU WA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA MAENDELEO YA NCHI" mbayo inalenga katika kuhakikisha kuwa watu wote wananpata fursa sawa ya kujua kusoma, kuhesabu na kuandika na maadhimisho haya kwa wilaya ya tunduru yatakuwa na manufaa sana kutokana na uwepo mkubwa wa watu wazima na vijana ambao hawajui kusoma nakuandika na wengine hawakupata fursa kutokana na ukosefu wa rasilikmali hasa fedha kutokana na elimu ilikuwa inatolewa kwa mfumo wa malipo.
Wanakisomo kutoka shule ya msingi Nalasi waliishukuru serikali kuwapelekea fursa ya kujiendleza kutokana na kupata changamoto kubwa sana hasa katika mawasiliano, miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao zinatolewa wanakosa kutokana na kutokujua kusoma na kuandika.
"unakuta kata bili ya maji unashindwa kusoma mpaka akaitwe jirani kuja kusoma wakati nyumbani nipo lakini kwa sababu sijui kusoma na kuandika inakuwa changamoto, kusoma meseji kwenye simu nayo ni shida vile vile, hivyo kwa mfumo huu wa kusoma kisomo cha manufaa kitatusaidia sana katika kupata haki zetu na hata kufanikiwa kiuchumi kwani ukiona watu waliosoma wana maendeleo zaidi ya wale ambao hatujasoma"
Darasa la kisomo katika kata ya mbesa la shule za msingi za Airpot na Mbesa wakimsikiliza Afisa Elimu watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi Mwalimu Musa Nkolabigawa wakati alipotembelea darasa hilo mapema wiki hii, katika maandalizi ya Maadhimisho ya Juma la Elimu ya watu wazima ambayo kilele chake kitafanyika wilyani Tunduru katika Mkoa wa Ruvuma Kitaifa tarehe 21.09.2017
Afisa Elimu watu wazima wilayani tunduru mwalimu musa nkolabigawa akizungumza na vijana ambao hawakupata fursa ya elimu ya msingi na sekondari katika kata ya nalasi mapema wiki wakati alipowatembelea kukagua utekelezaji wa uendelezaji wa madarasa ya elimu ya watu wazima kwa watu waliokosa nafasi ya kupata elimu ya msingi na sekondari katika wilaya ya Tunduru.
katika picha ni baadhi ya vijana ambao waliokosa fursa ya kupata elimu na wamejitokeza
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.