Hayo yamesemwa na Mganga mfawidhi hospitali ya wilaya ya Tunduru Dk Gaufredy Mvile wakati akiwapokea madaktari bingwa kutoka mkoani wa kutibu magonjwa ya kinamama
Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kupitia idara afya imeelendelea na zoezi la kutoa huduma za afya kwa jamii kwa kuendelea kuwaleta madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ili kusogeza huduma karibu za wananchi.
Akitoa taarifa ya ujio wa madaktari bingwa kutoka Mkoani Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya Dk Gaufredy Mvile alisema tumepokea madaktari bingwa kwa awamu mbili Kuanzia terehe 10/05/2017 hospitali ya wilaya imepokea madaktari bingwa wa magonjwa ya upasuaji kama Mabusha, Goita na Vimbe mbali mbali, pia walikuwepo madaktari bingwa walifanya uchunguzi wa magonjwa ya nje kama Pressure, Sukari, shinikizo la juu (hypertension)
Na wiki hii hospitali ya wilaya ya Tunduru imepokea madaktari bingwa wa magonjwa ndani ya kinamama hivyo wanatoa huduma kuanzia tarehe 12/06 hadi tarehe 16/ 06 2017 na watafanya uchunguzi kwa wagonjwa wenye magojwa makubwa kama vimbe na mengineyo ili kuwafanyia upasuaji.
pia hospitali imepokea waganga wa kufanya tohara kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 10 na kuendelea kwa sababu ni kundi ambalo lipo katika rika hatarishi kuweza kupata maambiki ya viruzi vya ukimwi na wakifanyiwa upasuaji unapunguza kwa asilimia 60 ya maambukizi.
Upasuaji huu unafanyika katika vituo mbalimbali ambavyo waganga watakuwepo klwa ajili ya kutoa huduma ya tohara, vituo hivyo ni nakapanya, nandembo, mkasale, mtina, huria, nalasi na katika hospitali ya wilaya.
Zoezi hili limefadhiliwa na shirika la WRP kwa kushirikiana na USA Aid wakiwa na lengo la kupunguza maambikizi mapya kwa vijana kwani vijana kuanzia miaka 10 na kuendelea ambao hawajafanyiwa tohara wako katika hatari kubwa ya kupata maambiki hivyo kuwafanyia upasuaji huo kwa asilimia kubwa serikali itafanikiwa kupunguza maabukizi alisema Dk Gaufredy Mvile.
Mganda mfawidhi aliendelea kusema kuwa kwa Tunduru wamepata changamoto kubwa sana kutoka na baadhi ya wazazi kuwaleta watoto walio chini ya miaka 10 hivyo kuleta usumbufu mkubwa kwa sababu shirika limewalenga kutoa huduma bure bila ya malipo kwa kundi lilotajwa.
Mganga Mfawidhi hospitali ya wilaya ya Tunduru Dk Gaufredy Mvile wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na waganga wa upasuaji wa tohara katika kampeni za kupunguza maambikizi ya Viruzi vya Ukimwi nchini inayoendeshwa na wizara ya afya jinsia wazee na watoto kwa kushirikiana na shirika la WRP na JHPIEGO. kutoka kushoto ni Dk kassimu malokotana, wa pili kutoka kushoto ni Dk Gaufredy Mvile mganga Mfawidhi (W), akifuatiwa na Dk pancras Komba na Dk Rose Mbawala wote kutoka wilaya ya Mbinga.
Imetolewa
Theresia Mallya
Afisa Habari (W)
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.