na Mwandishi wetu
Mkuu wa mkoa ametoa kauli hiyo jana, wakati akifungua soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito wilayani Tunduru ambapo alisema, kati ya fedha hizo shilingi ml 9,916, 254 zimetokana na mrabaha na shilingi ml 2.5 ni ushuru.
Mkuu wa mkoa alisema,tangu Serikali ilipoweka sheria ya kuanzishwa kwa soko la madini kumekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuongezeka kwa mapato ya Serikali na udhibiti wa madini ambayo kabla ya sheria hiyo kulikuwa na vitendo vingi vya utoroshaji madini na ukwepaji mkubwa wa kodi.
Alisema, katika kipindi hicho jumla ya gram 2824.2 zimepatikana kati ya hizo gram 2540 madini ya vito na dhahabu iliyopatikana ni gram 364.2.
Aidha Mndeme,ameagiza kufanyiwa ukaguzi wa mizani na vifaa vingine vya kupima madini hasa baada ya kubaini kuwa,baadhi ya vipimo vinavyotumika haviko sahihi jambo linaloweza kusababisha udanganyifu na hivyo kuikosesha Serikali taarifa mapato halisi.
Alisema, lengo ni kufahamu thamani ya madini yetu kwani kwa muda mrefu kumekuwa na udanganyifu mkubwa unaofanywa na wafanya biashara wa madini.
Alisema, ufunguzi wa soko la madini katika wilaya ya Tunduru na Songea mkoani humo ni utekelezaji wa Agizo la Rais Dkt John Magufuri ambalo linalenga kupata uhakika wa takwimu za madini,soko na uhakika wa bei na kuondoa unyanyasaji kwa wachimbaji wadogo unaofanywa na wanunuzi.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme aliyenyoosha mkono akiongea na baadhi ya wanunuzi wa madini ya vito mara baada ya kufungua soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito wilayani Tunduru jana ambapo ameagiza madini yote yanayochimbwa katika wilaya hiyo kuuzwa katika kituo hicho badala ya kuuzwa mitaani au nyumbani kwa wanunuzi.
Amewataka wananchi na wachimbaji wadogo wa madini katika mkoa huo kuwa walinzi wazuri wa rasiimali zetu za madini na kusisitiza kuwa yeyote atakayekamatwa anatorosha madini atachukulia hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani sambamba na kufutiwa leseni.
Hali kadhalika mkuu wa mkoa, ameziomba taasisi za fedha ikiwemo Benki kufungua huduma za fedha katika eneo la kuuzia madini ili kuwaondolea usumbufu wanunuzi na wauzaji madini kufuata fedha mbali sambamba na kuwataka wachimbaji wadogo kuhakikisha wanafungua Akaunti badala ya kutembea na fedha nyingi mifukoni jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.
Awali Afisa Madini mkazi wa wilaya ya Tunduru Juma Kapela alisema, wilaya ya Tunduru imebarikiwa kuwa na madini mbalimbali ya thamani kama Dhahabu,madini ya vito na shaba.
Kapela alisema, Ofisi ya Afisa madini mkazi inasimamia jumla ya leseni hai 342 za uchimbaji mdogo na imeshapokea maombi mapya yaliyopokelewa ni 56 ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini ambayo yapo katika hatua za kupitiwa kama yanakidhi vigezo ili yaweze kutolewa leseni.
Alisema, hadi sasa jumla ya leseni 239 zimepewa hati za makossa na leseni 1,342 zimefutwa kwa kutotimiza masharti ya umiliki wa leseni hizo kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa mkoa wa ruvuma akiwahutubia wananchi katika siku ya uzinduzi wa soko la dhahabu na madini ya vito wilayani Tunduru.
Alisema, kufunguliwa kwa Soko la madini katika wilaya ya Tunduru kutafungua milango kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini walioko katika wilaya ya Tunduru na maeneo jirani kupata sehemu ya kuuzia na kununua madini.
Kwa upande wao wachimbaji wadogo wa madini ,wamempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kukubali kukutana na wadau wa sekta ya madini ili kusikiliza kero za sekta ya madini.
Hata hivyo,wameiomba Serikali iweze kutengeneza mazingira mazuri ya soko la ununuzi wa madini ya vito kwa sababu wanunuzi hao wapo katika Kampuni tofauti hivyo kukaa chumba kimoja Zaidi ya mnunuzi mmoja inaondoa usiri wa Kampuni kwa Kampuni na mchimbaji anayehitaji kuiuzia.
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo wa Madini Mohamed Mlangwa alisema, hali hiyo inatokana na ukweli kwamba madini ya vito hayana bei maalum kama ilivyo kwa Dhahabu.
MWISHO
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.