“Serikali ya Jamhuri ya Tanzania inafanya jitihada za kila hali katika kumtua mwanamke ndoo lakini kuna baadhi wa wakandarasi wenye nia ovu wanaturudisha nyuma kwa kuchelewesha miradi ya maji”alisema mkuu wa mkoa wa Christina Mndeme akiwa ziarani Tunduru.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme akiwa katika ziara ya siku mbili wilayani Tunduru katika kata ya Mtina Jimbo la Tunduru Kusini wakati akikagua ujenzi wa miundombinu ya maji, mradi unaofadhiliwa na benki ya Dunia.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme (anayeangalia juu) akitoa maagizo kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji Mtina kufanya kazi hadi siku za jumamaosi na jumapili ili mradi huo kukamilika ndani ya muda wa mkataba ambapo
Alipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya utekelezaji wa mradi kwa kipindi cha takribani miaka sita bila kukamilika na kutoa huduma kwa wananchi hivyo kukwamisha azima ya serikali ya kumtua mama ndoo kichwani, na kuongeza uzalishaji ili kufikia uchumi wa kati ifakapo 2025.
Bi mndeme alimuagiza mhandishi wa maji wilaya ya Tunduru kuhakikisha kuwa mradi wa maji unakamilika kabla ya tarehe 18 octoba 2018 kulingana na mkataba na thamani ya fedha izingatiwe, alisema “naomba mpaka ifikapo octoba 18/2018 mkandarasi kukabidhi mradi huu na kasi ya utekelezaji inongezeke fanya kazi hadi siku za jumamosi na jumapili ili kumaliza kazi”
Mhandisi wa maji Halmashauri ya Tunduru Ndg Bartolomeo Matwiga akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji mtina kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme alipotembelea mradi huo akiwa katika ziara ya siku mbili wilayani Tunduru,
Mradi wa maji mtina ulianza kutekelezwa kuanzia mwaka 2013/2013 hadi sasa upo katika hatua za umaliziaji ambapo kumekuwa na changamoto nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuvunjwa kwa mkabata mwaka 2017 kutoka na mkandarasi kushindwa kutimiza masharti.
Mradi wa maji Mtina unaotekelezwa na kampuni Kihanga farm transport and general co.ltd unataraji kutoa huduma kwa wananchi wa vijiji vya Nyerere pamoja na Muungano vilivyopo katika kata ya Mtina .
Imeandaliwa
Theresia Mallya
Afisa Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.