Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imefanikiwa kutoa mkopo kwa awamu ya pili kwa ajili ya kuwezesha wanawake, vijana na walemavu ikiwa ni utekelezaji sera ya serikali ya kuhakikisha Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani inatenga fedha asilimia 10 kuwezesha makundi hayo.
Akitoa hotuba kabla ya kukabidhi hundi kwa makundi hayo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi alisema serikali inatekeleza yale yaliyopo katika sera na ilani ya chama tawala ya kuwawezesha wanawake, vijana na wenye ulemavu kiuchumi kwa kutoa mikopo isiyokuwa na Riba.
Mkurugenzi huyo alivitaka vikundi wanaokopeshwa fedha hizo kubuni miradi inayoendana na thamani ya fedha watakayopata ili iwe na tija kwa kubadilisha hali za maisha yao na familia kwani lengo ni kumuinua mwananchi kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi akikabidhi hudhi kwa vikundi vya wanawake, walemavu na vijana ya asilimia 10 ya mapato ya ndani katika uwezeshaji kiuchumi.
Gasper aliwaasa vikundi hivyo kutengeneza bidhaa zenye ubora na viwango,kwa kutafuta vifungashio vizuri na lengo ili kuongeza uthamani wa bidhaa wanazozalisha.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Ndg Balyomi aliwaagiza wataalamu mbalimbali kutembelea vikundi vijijini na kuona shughuli wanazofanya na kutoa elimu uzalishaji kwa vikundi “niwaagize wataalam wa Maendeleo ya jamii, Kilimo, Mifugo, FDC Nandembo na wengine tembeleeni vikundi vijijini kutoa elimu”
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Tunduru Gudluck Shirima akiongea na wanufaika wa mkopo wa asilimia kumi ya Halmashauri ambao hawapo kwenye picha kuwata kutumia fedha kujiendeleza kiuchumi.
Naye Kaimu Afisa maendeleo ya jamii Ndg Fadhili Chidyahaonga alisema kuwa Halmashauri imetoa mkopo kwa vikundi mara mbili na wanatarajia kutoa tena kwa mara ya tatu kabla ya mwaka wa fedha 2018/2019 kwisha.
Kwa upande wa meneja wa benki ya NMB tawi la Tunduru Ndg Goodluck Shirima aliviasa vikundi vinavyochukua mkopo kuwa na shunguli endelevu ili kujikomboa kutoka katika hali ngumu ya maisha, pia kufanya marejesho kwa wakati li vikundi vingine viweze kunufaika kama wao walivyopata mkopo huo.
Halmashauri ya wilaya ya Wilaya ya Tunduru kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 imetoa mkopo kwa vikundi 24 awamu ya kwanza wenye thamani ya 33,500,000 ulitolewa na awamu ya pili jumla ya shilingi 50,363,440 umetolewa kwa vikundi vya walemavu 5, vijana 13 na wanawake 14.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.