Jumuiya ya walimu wakuu na waratibu Elimu Kata wilayani Tunduru leo tarehe 26/10/2017 wamemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji (W) vifaa vya shule kwa wanafunzi waliounguliwa na Bweni katika shule ya Sekondari Nandembo, mapema wiki iliyopita bweni la wanafunzi wavulana lilingua moto na kuteketea kwa vifaa vya wananfunzi wakati wakiwa katika vipindi vya dini jioni.
akizungumza na wananfunzi wa shule ya sekondari nandembo mwakilishi wa jumuiya ya walimu na waratibu elimu kata alisema waliipokea taarifa hiyo kwa masikitiko na mshituko mkubwa sana kutokana na wanafunzi kupoteza vifaa vyote ikiwa ni pamoja na sare za shule, madaftari, magodoro na vifaa vyote vilivyokuwamo ndani ya bweni hilo.
alisema "tukio hili ni la kawaida linatokea mahali pengi hivyo utulivu uwepo ili muweze kusoma na kuendelea na ratiba za kawaida katika shule, niendelee kuwasihii kujisomea kwa utulivu hasa kidato cha nne wanaojiandaa na mitihani ya kidato cha nne ambayo inatarajia kuanza tarehe 30/10/2017"
akiongea na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari nandembo kuwafariji mkurugenzi mtendaji (W) Ndg Abdallah H. Mussa aliwapa pole sana wanafunzi kwa tukio la moto na kuwasihi wananfunzi kuondoa taharuki kwani jango hilo ni la kawaida na wanamshukuru mungu hakuna mwanafunzi alipata ajali
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.