Serikali yaendelea kuboresha mazingira ya shule zake.
katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Halmashauri ya Tunduru imeendelea kuweka kipaumbele katika shule kwa kuboresha miuondmbinu yake, kujenga madarasa,matundu ya vyoo na nyumba za kukaa wafanyakazi.
UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA NA OFISI KATIKA SHULE YA MSINGI TEMEKE.
Uongozi wa shule ya msingi Temeke unaendelea na ujenzi wa vymba 2 vya madarasa na ofisi baada ya kupokea fedha kutoka halmashauri jumla ya shilingi milioni 10,000,000.00 kwa kushirikiana na nguvu za wananchi.Shule imefanikiwa kujenga vyumba 2 vya madarasa ambapo ujenzi umefikia katika hatua ya kuezeka, kukamilika kwa madarasa haya kutapunguza mlundikano wa wanafunzi madarasani na kuboresha mazingira ya ufundishaji. Akizungumza na mkuu wa shule, mkuu wa msafara wa kamati ya uongozi, fedha na mipango wakati wa ukaguzi wa miradi inayotekelezwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 Mh. Wadali Mfaume Wadali ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri aliwaambia walimu wasimamie ujenzi huo kwa karibu ili ukalimilike kwa muda uliopangwa na Halmashauri.
UJENZI WA NYUMBA YA WALIMU SHULE MSINGI SAUTI MOJA.
Ujenzi wa nyumba ya walimu ya mbili kwa moja umekamilika katika Shule ya Msingi Sauti Moja iliyopo katika Kata ya Namakambale Wilayani Tunduru, ujenzi uligharimu jumla ya shilingi milioni 40 fedha za bakaa ya ruzuku ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2014/2015.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.