serikali kwa kuzingatia sera ya elimu bure na kuboresha miundombinu na mazingira ya kusomea wanafunzi na kupunguza changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu imeaznsha ujenzi wa hosteli moja katika shule ya sekondari semeni iliyopo kata ya Mtina wilayani Tunduru.
shule nyingi zilikua zinakumbwa na utoro shuleni hali inayosababishwa na wanafunzi kutmbea umbali mrefu.
Ili kukabiliana na changamoto ya wanafunzi kukatisha masomo Halmashauri katika bajeti ya mwaka 2016/2017 imetenga kiasi cha shilingi milioni 29,048,000.00 za kujenga bweni moja katika shule ya sekondari semeni.
Ujenzi wa bweni hilo utachangia kupunguza utoro wa wananfunzi na wanafunzi kukatiza masomo kutokana na kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani hadi shuleni.
vile vile kutaongeza kiwango cha ufaulu kwa wananfunzi kwani watakuwa wanakaa shuleni na kupata muda mwingi wa kujisomea tofautina hali ilivyo sasa wanatumia muda mwingi njiani muda ambao watatumia kufanya mazoezi.
ujenzi huo utarajiwa kukamilika ndani ya mwaka wa fedha 2016/2017, hatua liyofikiwa mpaka sasa ni uandaaji wa uwanja na wananchi wanaendelea kukusanya mchanga.
Akiongea na mkuu wa shule wakati wa ukaguzi wa Miradi makamu mwenyekiti wa halmashauri Mh Wadali Mfaume aliigiza kamati ya ujenzi ya shule ya sekondari Semeni kuhakikisha kuwa mradi wa ujenzi wabwni unakamilika kwa muda uliopangwa .
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.