Wakiwa katika mkutano wa mwaka wa jukwaa la kuwainua wanawake kiuchumi wilayani Tunduru uliofanyika katika ukumbi wa hospitali ya wilaya, Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wilaya Bi Jocelyne Mganga aliwataka wanawake kuwa na upendo, mshikamano na umoja ili kujiletea maendeleo kama wanawake wa wilaya nyingine.
Akizungumza na wanachama wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake Kiuchumi wilayani Tunduru, Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya wakati wa kufungua mkutano wa mwaka Mama Fatuma Mkina alisema wanawake wanatakiwa kubadilika ili kuweza kujikwamua kiuchumi kwani ni muda mrefu tumekuwa nyuma.
“sisi wanawake wa wilaya ya Tunduru tumebaki nyuma kwa kipindi kirefu ni muda sasa wa kuona fursa zilizopo na kujikwamua kiuchumi, tuache hofu ya kushindwa kwani wanawake wa mikoa mingine wamewezaje!na hata sisi tukiamua tunaweza” alisema mwenyekiti wa jukwaa.
Mama Akukweti akitoa hoja ya kufanyika uhamasishaji wa wanawake kujiunga na jukwaa la kuinua wanawake kiuchumi wilaya ya Tunduru katika mkutano wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa hospitali ya wilaya.
Akisoma taarifa katibu wa jukwaa la wanawake wilaya Bi Asigele Chonde alisema jukwaa linakumbwa na changamoto za ukosefu wa vitendea kazi, na ukosefu wa fedha kwa ajili ya kukopeshana hivyo kuchelewesha maendeleo kwa wanawake.
Bi Asigele Chonde aliendelea kutabainisha kuwa ili waweze kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa fedha jukwaa limeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchango wa shilingi 1000 kwa kila mwanamke kwa kila mwezi ambayo itawekwa katika akaunti ya jukwaa.
Na kwa upande wa mwanajukwa mama Akukweti aliwata viongozi wa jukwaa kuandaa ratiba ya kuzunguka katika kata na vijiji vyote vya wilaya ya Tunduru kufanya uhamasishaji wa wanawake kujiunga na jukwaa la wanawake, “kwani kama wilaya ya Tunduru ina takribani ya wanawake laki mbili (200,000) ni dhairi kwamba kama wote watajiunga na jukwaa mapato yatakuwa makubwa na kuwezesha kupata mikopo kwa urahisi na kuinuana kiuchumi”
wanawake wakifuatilia mkutano wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi uliofanyika katika ukumbi wa hospitali ya wilaya tarehe 01.septemba 2018.
Aliendelea kusema kuwa ni vyema kuwatumia hata viongozi wa umoja wa wanawake wa chama katika kata na mashina UWT ili kuwafikia wanawake wengi zaidi.
Hata hivyo mkutano ulifikia maazimio ya kila mwanamke kuchangia shilingi 1000 kila mwezi, na ada ya kiingilio shilingi 3000 kulipwa mara moja kwa kila mwanamke/ mwanachama wa jukwaa la wanawake.
Imetolewa na
Theresia Mallya
Afisa Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Tunduru
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.