Akiwa katika ziara ya siku moja wilayani Tunduru Naibu Waziri wa wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Eng Stella Manyanya alipokea taarifa ya maandalizi ya msimu wa korosho kwa mwaka 2018/2019 ambao umezinduliwa tarehe 01/10/2018, alisema ni vyema Bodi ya Korosho Tanzania kuhakikisha mahitaji muhimu yanapatikana kwa vyama vya msingi kwa wakati ili kupunguza malalamiko na changamoto za msimu uliopita.
Aidha Naibu waziri Eng Manyanya alitembelea maghala manne yaliyoteuliwa kuhifadhi korosho ghafi kwa msimu kwa mwaka 2018/2019 ambayo ni ghala la halmashauri ya Tunduru, ghala la chama kikuu cha ushirika (TAMCU), ghala la Poa Rice Mill na ghala la forward.
Naibu waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Eng Stella Manyanya aliyevaa kitenge akitoa maelekezo kwa mkandarasi ya ufanya marekesho kwenye upandishaji wa Kuta ili kufanya mradi uwe na ubora unaotakiwa.
Vilevile naibu waziri alitembelea ujenzi wa ghala kubwa la serikali linalojengwa kwa thamani ya shilingi bilioni 5 chini ya usimamizi wa Bodi ya Korosho Tanzania kuona changamoto zinazokabili utekelezaji wa mradi huo ambao umekuwa ukisuasua kutokana na sababu mbalimbali.
Eng Manyanya akiwa katika eneo la ujenzi wa ghala alipokea taarifa kutoka kwa mkandarasi ndugu YEKA HAMISI alisema wamekuwa wanakumbana na changamoto ikiwa ni pamoja na ucheweshaji wa fedha kutoka serikalini, ukosefu wa saruji kutokana na kiwanda cha Dangote kusimamisha uzalishaji, na masika yaliathiri kazi kwa kipindi cha January hadi machi. “tunaimba serikali kuleta fedha kwa wakati kwani changamoto kubwa imekuwa fedha kutokufika kwa wakati na zikifika ni kiwango kidogo ukilingana na tulichoomba” alisema
katika Picha ni Naibu waziri wa Viwanda, Bishara na Uwekezaji Eng Manyanya akifanya ukaguzi wa mradi unaokelezwa kwa usimamizi wa Bodi ya Korosho nchi wenye thamani ya shilingi Bilini 5. kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Homera, Katika ni Naibu waziri wa Eng Stella Manyanya na kushoto ni Mhandisi Yeka Hamisi.
Eng Manyanya alisema ufuatiliaji utafanyika ili fedha ziweze kuletwa kwa wakati na pia aliomba mradi wa ujenzi wa ghala kukamilika kwa wakati ili kutoa fursa kwa wananchi kutunza korosho zao katika mazingira safi na salama na kwa ubora wa hali ya juu.
Eng Stella Manyanya akitoa maagizo ya Mmoja wa watunza ghala kwa msimu wa korosho 2018/2019 ndg Forward (aliyevaa saa Mkononi) alipotembelea katika ghala lake ambalo limeteuliwa kuhifadhi korosho.
Hata hivyo Eng manyanya alitoa Onyo kali kwa watunza ghala juu ya suala la unyaufu na uchafu kama mawe na mchanga katika korosho, “seikali haitosita kuchukua hatua kwa watunza ghala ambao watasabisha usumbufu kwa wananchi au kushiriki katika suala la rushwa ili kupokea na kuhifadhi ghalani.”
Imeandaliwa na
Theresia Mallya
Afisa Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Tunduru
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.