Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la uhifadhi wa Mazingira pamoja na Wanyamapori, Protected Areas Management Solution (PAMS), wametoa Elimu kwaWanafunzi wa shule ya Sekondari Nampungu kuhusu uhifadhi wa mazingira, wanyamapori, na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Akizungumza na Wanafunzi hao, Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Jecelyne Mganga aliwataka Wanafunzi hao kuzingatia Elimu na kuwa na nidhamu kwa jamii inayowazunguka. Aliwasisitiza kuachana na mambo yatakayosababisha kushindwa kutimiza malengo yao ya baadaye.
Sambamba na hilo ,Ustawi wa Jamii wakishirikiana na Dawati la Jinsia na Watoto walitoaa Elimu juu ya Ukatili wa kijinsia , na namna ya kuweza kukabiliana na ukatili huo na wapi wanaweza kwenda kupata msaada wa haraka kutoka na athari za ukatili, pamoja na haki a wajibu wa Mtoto katika Jamii.
“Elimu ni ufunguo wa Maendeleo Endelevu , tunapaswa kuizingatia yale tunayoyapata kutoka kwa walimu wetu”. Alisema Bi. Mganga “Tunzeni utu wenu ,ili muweze kutimiza ndoto zenu”.
Aidha Ndg. Oscar Bakumbezi Mratibu Mradi PAMS Wilaya ya Tunduru akishirikiana na Bi. Asha, Askari wa uhifadhi kutoka jumuiya ya Chingoli na Narika Wilaya ya Tunduru Amezungumza na wanafunzi kuhusu utunzaji bora wa Mazingira na Wanyamapori.
Akizungumza na wanafunzi hao Bi. Asha alisema Elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira na wanyamapori ni muhimu sana kwa vijana, kwani ndio watakaokuwa na jukumu la kulinda rasilimali hizi kwa ajili ya vizazi vijavyo.
PAMS inafanya kazi nzuri kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii kuwafikia wanafunzi na kuwapa maarifa na ujuzi wanaohitaji ili kuwa watunzaji bora wa mazingira. PAMS, kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jami pia walikabidhi Taulo za kike kwa wanafunzi wa kike.
Mwanafunzi Zurea Ahamdi Ngaunje, kwa niaba ya wanafunzi wenzake, alishukuru Idara ya Maendeleo ya Jamii na PAMS kwa elimu iliyotolewa kuhusu uhifadhi wa mazingira, wanyamapori, na maendeleo ya jamii.pia kwa kukabidhiwa Taulo za kike zitakazowasaidia katika kutimiza ndoto zao za kitaaluma.
Ushirikiano kati ya Idara ya Maendeleo ya Jamii, PAMS, na wadau wengine wa maendeleo ni jambo la kuigwa katika kuhakikisha vijana wanapata elimu bora kuhusu mazingira na jamii
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.