Dkt. Mwakyembe Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amewataka Wananchi wa Wilaya ya Tunduru kata ya Masonya watunze mahandaki na majengo ya kihistoria yaliyopo katika kata hiyo ya masonya ambayo yalitumiwa na Wanachama wa FRELIMO katika kupigania Uhuru wa Nchi ya Msumbiji pia Mhe.Dkt. Mwakyembe alisema Serikali itakarabati maeneo hayo ya kihistoria kwajili ya vizazi vijavyo.
Katika kuboresha mazingira hayo na uhifadhi wa Malikale Dkt. Mwakyembe alisema kuwa serikali itashirikiana na serikali ya Jamhuri ya Msumbiji katika kuboresha maeneo hayo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa malikale zilizotumiwa na wanaharakati wa FRELIMO ili kutunza historia na kuwaenzi waasisi wa ukombozi wa Nchi hiyo na kutambua mchango wa Tanzania katika ukombozi wa nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara.
aidha alipata fursa ya kutembelea na kukagua majengo mbalimbali yalitumiwa na wanaharakati wa Msumbiji, maeneo ya mahandaki na uwanja uliotumika na umoja wa wanawake wa Msumbiji katika harakati za ukombozi mwaka 1973 kufanya mkutano wa kwanza baada ya umoja huo kuanzishwa.
Katika picha kulia ni waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harson Mwakyembe akitoa maelekezo ya namna ya uboreshaji wa eneo la masonya wakati alipofika kwenye mnara wa uwanja wa umoja wa wanawake wa Msumbiji katika eneo la makumbusho ya Masonya.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.