Ded Tunduru dc kutoa milioni miambili na arobaini 10%.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg Gasper z. Balyomi leo tarehe 01/04/2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Wanufaika wa mkopo wa Halmashauri wa 10% ambao wanufaika hao ni Wanawake 4%, Vijana 4% na Walemavu 2% ambapo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru amewataka wananchi wajiunge katika vikundi ili wanufaike na mkopo huo wa Halmashauri.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru amewataka vikundi ambavyo wamekopa mkopo na hawajaresha mikopo yao anawataka vikundi hivyo warejeshe mikopo kwa wakati ili kuwapa fursa na vikundi vingine wakope.
Pia Mkurugenzi Mtendaji amesema “kwa vikundi ambavyo vinakopa na kurejesha mikopo yao kwa wakati vitapewa kipaumbele na kuongezewa kiwango cha mkopo” ambapo kwa sasa kuna vikundi vinarejesha vizuri sana marejesho.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Tunduuru imetenga kiasi cha shiling milioni mia mbili na arobaini kwajili ya kuwakopesha Wanawake 4%, Vijana 4% na Walemavu 2% ambayo ni asilimia kumi (10%) inayo takiwa kutolewa kwa Wanawake, Vijana na Walemavu kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa serikali pia Mkurugenzi amewapongeza vikundi vya Wanawake kwa kuonyesha mwenendo mzuri wa kurejesha mkopo huo katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.