Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndg. Chiza Marando, ameendesha kikao cha kawaida cha kujadili utekelezaji wa shughuli za lishe kwa robo ya kwanza (Julai – Septemba 2023) katika Wilaya ya Tunduru Novemba 10,2023, ambapo alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa kikao hicho amewasisitiza wakuu wa idara ambazo zinawajibika katika kamati ya Lishe kuendelea kuonesha ushirikiano kwa kamati ya lishe ili kuongeza hali nzuri ya lishe katika wilaya ya Tunduru,na kuwataka kwenda kutekeleza makubaliano katika kila idara husika.
Ameyasisistizaa hayo wakati wa kikao hicho ofisini kwake, ambapo pia aliziomba idara za Elimu kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na mwenendo mzuri wa Lishe wawapokuwa shuleni , kwani lishe bora ni msingi wa maisha ya binadamu.
Pichani Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Tunduru Ndg. Chiza Marando akizungumza wakati wa kikao cha Utekelezaji wa masuala ya Lishe ofisini kwake.
“Ninyi kama wakuu wa idara zinazohusiana na masuala ya lishe hakikisheni mnatimiza wajibu wenu katika kuhakikisha lishe kwa wananchi wa wilaya ya Tunduru inakuwa Bora”
Kwa upande wake Afisa Lishe Wilaya ya Tunduru Bi. Martha Kibona aliwasilisha taarifa ya Idara ya Afya kwa niaba ya Mganga Mkuu wa (W) Tunduru , ambapo idara ya Afya ilitekeleza kwa utoaji elimu mbalimbali kwa rika balehe na elimu juu ya ulishwaji wa watoto wachanga na wadogo pamoja na uongezwaji wa virutubishi katika vyakula.
Pichani (aliyesimama) Afisa Lishe wilaya ya Tunduuru Bi. Martha Kibona akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa masuala ya Lishe katika Idara ya Afya.
Afisa Afya (W) Tunduru ameendelea kuhamasisha viwanda kuingia mkataba na SANKU kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa vyakula vyenye virutubishi vya kutosha.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.