Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw. Julius Sanday Mtatiro amezitaka Taasisi za mkopo kuto wazurumu watumishi wastafu kama ilivyo fanya taasisi za mikopo ambazo zimemzurumu mwalimu mstaafu Bw.Kanyita Abdalah Mruta ambapo alizurumiwa Zaidi ya milioni hamsini na tisa na taasisi hizo
Aidha Dc Mtatiro amewashukuru sana Takukuru kwa kuweza kufuatilia swala hiloa na kuweza kuwatia nguvuni wa tuhumiwa wote ambao walihusika katika kudhurumu haki ya Mwalimu huyo mstaafu ambae alinza kazi mwaka 1980 na kustaafu 2018 ambapo asilimia 80 ya pesa yake ya kustaafu imeporwa na taasisi hizo za mikopo
Pia Dc Mtatiro amewataka watumishi wengine ambao wamedhurumiwa na taasisi hizo za mikopo waje ofisini kwake ili waangalie namna ya kuwasaidia haraka kwa kushirikiana na Takukuru wilaya ya tunduru aidha Dc Mtatiro amewataka watumishi wa tunduru wajifunze kutokana na makosa waangaliege na taasisi za kukopa maana taasisi hizo zipo kisheria lakini zina kiuka mashariti za mikopo inakopesha kwa riba kubwa adi riba mia sita(600) kitu ambacho kisheria hairusiwi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.