Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Julius S. Mtatiro, ametoa wito kwa madereva, abiria, wasafiri na wananchi wote kuwa wavumilivu kutokana na hali ya Mto Muhuwesi kujaa maji na kushindwa kupitika kwa magari.
Hali hii imeathiri usafiri kuelekea Mtwara, Dar es Salaam, Lindi na Pwani Na kutoka katika mikoa hiyo kuelekea Tunduru, Namtumbo, Songea Njombe, Iringa na Mbeya.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika Daraja la Mto Muhuwesi, Mheshimiwa Mtatiro amesema kuwa usalama wa wananchi ni kipaumbele cha kwanza cha serikali, pia ametoa wito kwa Wahandisi wa TANROADS kufanya ukaguzi wa kina wa daraja hilo baada ya maji kupungua kabla ya kuruhusu magari kupita.
"Ninaomba radhi kwa usumbufu wowote unaoweza kutokea kutokana na hali hii. Tunaomba wananchi wawe wavumilivu wakati tunasubiri maji kupungua na TANROAD kufanya ukaguzi wa daraja. Usalama wa wananchi ni kipaumbele cha kwanza cha serikali," Mheshimiwa Mtatiro amesisitiza.
Mheshimiwa Mtatiro ametoa wito pia kwa wananchi kuepuka kuvuka mto kwa miguu wakati maji yamejaa kwani ni hatari, Amewahakikishia Madereva na Abiria usalama wa mali zao wakati wa kipindi chote watakapokuwepo katika eneo hilo.
Kwa niaba ya Madereva wa Magari yaliokwama kutokana na kadhia hiyo, Ndg. Fabian Ignas Mnyenyelwa Dereva wa magari makubwa ya kusafirisha Makaa ya Mawe, amesema kadhia hiyo inawaathiri kwani wametumia muda Mrefu katika eneo hilo ambalo halina huduma za kijamii, pia ameiomba serikali kufanyia marekebisho Daraja hilo , ikiwezekana kwa kuliinua zaidi ya kina kilichopo kwa sasa.
Aidha kwa upande wao wananchi wa Kijiji cha Muhuwesi wamesema kujaa kwa daraja hili kunapelekea kusimama kwa shughuli za kijamii na kiuchumi kuna wananchi wapo upande wa pili wa daraja ambapo walikwenda mashambani na wameshindwa kurejea kutokana na kujaa maji ktikaa Daraja hilo
Hali ya Mto Muhuwesi imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na mamlaka husika, na taarifa zaidi zitatolewa pindi hali itakapobadilika.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.