Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mh. Juliusu Mtatiro amewaagiza Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru waongeze juhudi ya kubuni vyanzo vipya vya mapato lengo kuongeza wigo wa kukusanya mapato katika Halmashauri ya Wilaya Ya Tunduru amesema hayo wakati alipo alikwa kwenye baraza la robo ya Nne ya Mwaka fadha 2021-2022.
Dc Mtatiro aliwapongeza Waheshimiwa Wabunge, madiwani na Wataalam kwa Ujumla wao kwa ushirikiano walio uonesha na kuiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kuweza kufikia Malengo na kupata Hati safi kwa Mwaka wa Fedha 2021-2022.
Pia alitolea ufafanuzi wa swala la ugawaji wa pembejeo linavyo endelea aliseama”Zoezi la ugawaji Pembejeo kwa msimu huu wa Kilimo linaendelea vizuri kwa ushirikiano wa Kamati mbalimbali zilizo undwa kwa mujibu ya mwongozo kuanzia ngazi ya Wilaya adi ngazi ya Kijiji hivyo pale inapo tokea tatizo kamati hizo uwasiliana na kuzitatua kwa wakati”.
Kuusu Sensa Dc Mtatiro amesema “ Sensa ya mwaka huu 2022 kwa Tunduru ni Sensa ya kihistoria kwani Hamasa ilikuwa kubwa na zuri mwitikio wa Watu ni mkubwa sana kwani Wananchi wa Tunduru hawapendi kurudia tena makosa ya Mwaka 2012 ambapo makosa hayo yanatufanya Wananchi wa Tunduru tuteseke adi sasa kwani mwaka huo idadi ya watu ambao walikubali kuesabiwa kwa Tunduru walikuwa Wachache sana tofauti na Uhalisia hivyo ni matumaini yangu kwa Sensa hii ya 2022 Tunduru tutaongoza katika mkoa wa Ruvuma”.
Ishu ya Wafugaji Dc Mtatiro aliseam “Ofisi yake imejipanga kuendeleza Msako wa kuondoa wafugaji holela pasipo kumuonea mfugaji yeyote Yule kikubwa kila mfugaji aelekee kwenye kitalu alicho pangiwa na sio vinginevyo endapo Mfugaji akikamatwa yupo nje ya Eneo la kitalu chake atapigwa faini kila Ng’ombe elf ishirini (20,000) pesa hiyo ya adhabu itaingia Halamashauri kwa lengo ya kwenda kujenga miundombinu ya Jamii hapo lengo kubwa ni kupunguza Migogoro ya Wakulima na Wafugaji.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mh. Hairu Hemedi aliwaomba Waheshimiwa Madiwani na Wataalam kuendelea kushirikiana katika kuijenga Halmashauri ya Wilaya yaTunduru katika kuongeza mawazo ya Kubuni vyanzo vya Mapato Vipya ambapo Halmashauri ikikusanya mapato katika Vyanzo hivyo vipya itaongeza wigo wa kutoa Huduma kwa jamii ya Wanatunduru ikiwemo kujenga Zahanati na Madarasa katika sehemu mabalimbali katika Halmashauri ya Tunduru.
Mwisho, Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mh. Hairu Hemed Mussa aliwaagiza Waheshimiwa Madiwani akiwataka wakashirikianae na Wataalam waliopo kwenye Kata zao wakahakikishe Wanasimamia ipasavyo Swala zima la kukusanya Mapato kwani kwa kupitia Mapato ya Ndani Halmashauri utoa asalimia 60 kwa lengo la kujenga miradi mabalimbali ya maendeleo ambapo miradi hiyo ujengwa uko uko Wanako ishi Waheshimiwa Madiwani.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.