Mh.Dc Mtatiro amesema kwa sasa serikali inaendelea na mpango wake wa kuhakikisha kila mwananchi wa Halmashauri ya Tunduru anapata Bima ya afya kwa Tshs 30000/=Tu ambayo itamsaidia mwananchi kupata matibabu katika hospitali zote za rufaa ndani ya mkoa
Aidha Mkuu wa wilaya Julius Mtatiro amewataka wananchi wa Kata ya Azimio,Mbati na Mchoteka kuwa msimu wa korosho umeanza na mnada wa kwanza utafunguliwa tarehe nane mwezi wa kumi kwa Wilaya ya Tunduru hivyo ni vyema wananchi wakiuza korosho wahakikishe wanakata Bima ya afya kwa Elf 30 tu
Pia Mh. Mkuu wa Wilaya aliwaeleza Wananchi faida za kumiliki Bima ya Afya kwamba faida ya kwanza katika bima ya Afya kuna wategemezi wanne (4) ambao wata kuwa wanatumia pamoja na mmiliki wa bima ya Afya, faida ya pili kwa mwananchi anae miliki bima ya afya anakuwa mwenye furaha sana na mwenye kujiamini kuliko ambae mwanachi hana bima ya afya
Mh. Mkuu wa Wilaya Julius Mtatiro amewambia Wananchi kuwa afya ni mtaji hivyo amewataka kila mwananchi hakikishe anakata bima ya afya kwani ugonjwa au matatizo ya kiafya yanapo kuja hayana taarifa muda na wakati wowote mtu anaumwa haijarishi kama una pesa au huna pesa hapo ndipo umuhimu wa bima ya afya uonekana hivyo amewataka kila mwananchi akate bima ya afya kwa elf 30000/=tu kwa mwaka.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.