Mh. Julius Mtatiro anaendelea kutekeleza Ahadi zake ambazo alizitoa waKati wa Ziara yake ya kikazi ambayo alitembelea kusikiliza kero za Wananchi wa Wilaya ya Tunduru yenye Tarafa 7,kata 39 na Vijiji 157
Mkuu wa Wilaya alisema kuwa fedha na vifaa vya ujenzi anavyo toa kwa Wananchi ni sehemu tu ya Ahadi zake ambazo aliwaahaidi Wananchi wakati akiwatembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyo buniwa na wananchi wa vijiji na kata uhusika.
Pia aliwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wa Tunduru kasikazini na Tunduru kusini kwa Ushirikiano wanao uonyesha kwa Wananchi kwani Wabunge wa Tunduru kasikazini na Kusini wamekuwa wanashiriki kikamilifu kwenye miradi ya Maendeleo inayo tekelezwa kwenye majimbo yao.
Mkuu wa Wilaya alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndugu Chiza Marando kwa kuweza kusimamia vizuri miradi ya Maendeleo inayo endelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwani pale inapo onekana kuna tatizo amekuwa wanawasilina na kuangalia namna ya kutatua tatizo linaloonekana ni kikwazo katika mradi husika.
Aidha Kwaniaba ya Mbunge wa Tunduru kasikazini Mh. Hassani Kungu akitoa salamu za pongezi kwa Mkuu wa Wilaya Katibu wa Mbunge Bw.John Floteo alisema ofisi ya Mbunge Tunduru Kasikazini inatambua mchango mkubwa wa Maendeleo unaofanywa na Dc. Mtatiro kwa Jimbo lake kikubwa amemuomba waendelee kushirikiana kwenye Shida na raha katika kuhakikisha Wananchi wa Tunduru kasikazini Wanaendelea kupata maendeleo kwa kasi kubwa Pia akitoa salamu za Mbunge wa Tunduru Kusini Bw.Hamadi Seif alisema ofisi ya mbunge inamshukuru sana Dc kwa kutoa msaada wa mifuko ya Saruji ya Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Mbati kwani Mh.Mbunge anatarajia kufanya ziara katika kata hiyo ya Mbati hivyo ofisi yake inampongeza kwa kutekeleza ahadi yake.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.