Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius S. Mtatiro amemkabidhi ofisi Mkuu wa Wilaya Tunduru Mhe. Simon K. Chacha na kumueleza changamoto ambazo anatakiwa kuzifanyia kazi.
Makabidhiano hayo yaliofanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Machi 14, 2024, ambapo yalihudhuriwa na wajumbe wa kamati ya Usalama pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wilaya ya Tunduru.
Mhe. Mtatiro aliwaomba Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Watumishi wa Halmashauri ya Tunduru kumpa ushirikiano Mkuu Wilaya ya Tunduru Mhe. Chacha. Akieleza kuwa mafaniko aliyoyapata kwa kipindi alichoongoza Wilaya ya Tunduru ni matunda ya ushirikiano waliompatia, hivyo ni muhimu wakaendeleza ushirikiano huo kwa Mkuu huyo wa Wilaya.
"kwa hakika, nipende kuwashukuru kwa ushirikiano mulionesha katika kipindi chote nilichokuwa nanyi, ombi langu kwenu muendeleze ushirikiano huu kwa Mhe. Simoni Chacha, kwani maendeleo katika Wilaya ya Tunduru yataletwa kutokana na ushirikiano Miongoni mwetu”.Alisema Mhe. Mtatiro.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Simon Kemori Chacha, amempongeza Mkuu wa Wilaya aliyetangulia na kusema atayaendeleza yale ambayo yaliachwa na Mkuu wa Wilaya huyo.
Mhe. Chacha mara baada ya kukabidhiwa ofisi, ameahidi kuendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake na kusisitiza ushirikiano, kwani Ofisi yake iko wazi kupokea ushauri wenye lengo la kujenga na kuiletea maendeleo zaidi Wilaya ya Tunduru.
“Nami natamani kufanya kazi kama vile mulivyokuwa mnafanya na kiongozi wetu alietangulia, pale ulipoishia nami nitaanzia hapo, Najua Bila ushirikiano hakuna maendeleo yatayoonekana”.Alisema Mhe. Chacha.
Kufuatia Uteuzi na mabadiliko ya viongozi mbalimbali ikiwemo wakuu wa Wilaya Mhe. Simon Kemori Chacha Likuwa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, ambapo kwa sasa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, na Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Julius S. Mtatiro amehamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.