Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Tunduru Adv.Julius S. Mtatiro amewataka watumishi madaktari na wauguzi wa wilaya kutokana na changamoto mbalimbali katika vituo vyao vya kazi vya kutolea huduma za afya amewaomba kuandaa vipaumbele vyao kati ya zile changamoto walizo wasilisha katika mkutano ulioitishwa na mkuu wa wilaya kuzungumza na madaktari na wauguzi wa wilaya ya Tunduru.
Pia katika mkutano huo uliudhuriwa na meneja wa Tanesco Tunduru Ndg.Joseph K.Mtula, alitoa ufafanuzi kuhusu suala la kufikisha umeme baadhi ya maeneo vituo vya kutolea huduma za afya, na aliahidi Tanesco kupitia wakala wa umeme vijijini REA wameendelea kufanya tathimini ya ufikishaji umeme katika vituo hivyoo vya huduma ya afya.
Pia meneja wa RUWASA Tunduru Eng.MAUA JOSEPH NGALLAH ametolea ufafanuzi kuhusu upelekaji wa maji safi na salama katika vituo vya huduma za afya, amesema kuna visima 15 vinatarajiwa kuchimbwa katika maeneo tofauti katika wilaya ya Tunduru na kuhaidi miradi hiyo itakuwa utatuzi wa tatizo ilo la maji katika vituo hivyo vya kutolea huduma ya afya.!
Mkuu wa wilaya amemtaka mganga mkuu wa wilaya kushughulikia watumishi wote wanaoonekana kuwa ni walevi katika eneo la kazi ili kuzidi kuboresha utendaji kazi katika idara ya huduma za afya .
Amewasihii watumishi wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa katika vituo vya utoleaji hudima za afya kuacha mara moja kabla hatua za kisheria kuchukuliwa .
Mwisho amewapongeza watumishi wote wa huduma za afya kwa moyo wao wa kujitoa kwa uzalendo na mshikamano katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika kuhakikisha huduma inayotolewa ni bora na uhakika mkubwa, na kuwataka kuendeleza umoja na mshikamano katika eneo la kazi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.