Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw. Julius Mtatiro akiwa ziara kata ya Chiwana,kijiji cha Mkandu ambapo wananchi walimweleza Tatizo la mipaka kati ya kijiji cha mkandu na kijiji cha Chiwana pia swali jingine lilihusu kuusu upungufu wa nguzo za umeme wa rea.
Dc Julius Mtatiro alianza kujibu swali la utata wa mipaka kati ya kijiji cha Mkandu na Chiwana alisema “ninaunda kamati ambayo itaongozwa na Afisa tarafa na wajumbe wengine ni mtendaji kata ,watendaji wa vijiji ,wenyeviti wa vijiji na mratibu elimu kata ya Chiwana”.
Aidha Mkuu wa wilaya Bw. Julius Mtatiro amewapatia siku 30 kamati hiyo aliyoiunda ambapo Mkuu wa wilaya amesisitiza kamati hiyo impatie majibu ndani ya siku 30 uku wakapitie dokumenti zote za vijiji hivyo ili kupata ushaidi uliojitosheleza.
Pia Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw.Julius Mtatiro alijibu swali la pili linalo husu upungufu wa nguzo za umeme alisema “lengo la serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha vijiji vyote 154 vilivyopo katika wilaya ya Tunduru vinafikiwa na huduma ya umeme wa Rea hivyo kwa kijiji cha Mkandu nguzo tayari zipo barabarani zinakuja hivyo muda wowote kuanzia sasa nguzo hizo zitawasili kijiji cha mkandu ili wananchi waunganishiwe umeme kwa bei ya Tshs 27000=Tu”.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw Julius Mtatiro ameaidi kutoa mifuko 25 ya saruji ikiwa ni juhudi ya kuunga mkono jitiada za wananchi wa kijiji cha Mkandu katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha mkandu hivyo mkuu wa wilaya amewataka wananchi wa kijiji cha mkandu waendelee kuwa wabunifu katika kubuni miradi ya maendeleo katika kijiji chao.
Pia Mkuu wa wilaya alizungumzia kuusu wafugaji wenye makundi makubwa ya wanyama aina ya ng’ombe alisema “Wafugaji wote wenye makundi makubwa ambao wapo hapa kata ya chiwana na wanaishi na mifugo yao kikubwa watambue kuwa hapa chiwana hakuna kitaru cha wafugaji hivyo opresheni itavyo kuja lazima tutawaondoa hivyo ni vizuri warudi katiaka vitaru vyao ambavyo wamepangiwa “.
Aidha Mkuu wa wilaya amewashukuru sana wananchi wa kijiji cha mkandu kwa mapokezi mazuri na upendo wa dhati walio uonyesha kwake amewahidi kuwa atarudi tena kijiji mkandu mwezi ujao kupeleka mifuko 25 ya cement ambayo ameaidi na kuangalia hari ya ujenzi wa zahanati hiyo ya kijiji cha mkandu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.