Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Matatiro alihudhuria katika mkutano maalum wa unadishwaji wa ghala ulioitishwa na Chama kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU LTD), Septemba 12, 2023 katika ukumbi wa Skyway uliopo mjini Tunduru.
Mheshimiwa Mtatiro alialikwa kama mgeni rasmi katika mkutano huo, ambapo alizungumza na wanaushirika kuhusu masuala mbalimbali ya Ushirika
Akizungumza katika mkutano huo Mh. Mtatiro alivipongeza vyama vya msingi kwa usimamizi mzuri wa shughuli za Ushirka ukilinganisha na hapo awali, pia alikipongeza Chama Kikuu cha Ushirka kupitia bodi yake ya uongozi kwa usimamizi wenye tija katika Ushirika.
Aidha Mh. Mtatiro ameipongeza TAMCU LTD kwa uamuzi mzuri na wenye tija wa kuamua kununua ghala lenye uwezo wa kuhifadhi mazao ya wakulima hadi Tani 5000 kwa wakati mmoja,pia amekitaka Chama kikuu kuendelea kuwekeza katika miradi ambayo itawezesha Chama kupata mapato kutoka vyanzo vingine, na si kutegemea tozo ya mazao pekee.
“Hiki mnachoenda kukifanya ni kitu kikubwa na muhimu sana, Muendelee kuikuza TAMCU, panueni uchumi wenu, ninyi ndio wana Ushirika” Alisisitiza.
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya ameitaka Idara ya kilimo kuendelea kutafuta Mbegu bora na sahihi ili kuongeza tija kwa wakulima katika mazao haya ya kimkakati, pia kupata ushauri bora toka kwa wataalamu wa kilimo ili kufanya kilimo bora na kisasa katika kuongeza uzalishaji wa mazao hayo .
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.